Header Ads Widget

MAGARI YA KUBEBA WANAFUNZI (SCHOOL BUS) YAKAGULIWA, MADEREVA WAONYWA

 


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Jeshi la polisi Usalama barabarani leo limefanya ukaguzi kwa magari yanayobeba wanafunzi 100 katika viwanja vya mnazi mmoja na kubaini baadhi ya magari hayakidhi vigezo vya kubeba wanafunzi.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi la ukaguzi likiendelea Kamanda wa Usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa ni vyema wamiliki wa magari yao kuhakikisha wanayafanyia ukarabati mara kwa mara Ili kuhakikisha magari hayo yapo salama kwa ajili ya kupunguza ajali za barabarani.


"Leo tumefanya ukaguzi wa magari 100, tutaendelea na ukaguzi huu mpaka September 5 Ili tuhakikishe magari yote yapo salama, na endapo gari ambalo halijakaguliwa halitaruhusiwa kuingia barabarani na ikitokea wamekaisi agizo hili basi tutawachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria"amesema Kamanda Mutafungwa.



Amesema kuwa, lengo la kufanya ukaguzi huo kwa Magari hayo ni kukagua  mifumo mbalimbali ikiwemo uchakavu wa bodi,Mfumo wa breki, matairi,mpangilio wa viti pamoja na mikanda yakujiunga wanafunzi wakiwa katika safari ya kuenda na kurudi shuleni.


Aidha, amesema kuwa wameamua kufanya ukaguzi kwa kipindi hiki ambapo shule zimefungwa ili kuhakikisha ifikapo Septemba 5 siku ya Shule kufunguliwa magari yote ambayo yamekutwa na kasoro yaweze kutengenezwa au kuondolewa Barabarani.



"Wazazi,wamiliki wa shule,wasimamizi wa watoto,wakuu wa shule pamoja na madereva kushirikiana na jeshi la usalama barabarani katika kuzuia hizi ajari,hivyo nawataka wamiliki wahakikishe magari ya Shule yanafanyiwa ukaguzi mara mbili Kwa mwaka kama sheria inavyoelekeza" amesema Mutafungwa 


Aidha, amewataka madereva ambao hawana leseni daraja C kwenda chuo cha Taifa cha Usafirishaji ( NIT) na Chuo Cha Elimu ya  Mafunzo ( VETA) Ili waweze kukidhi vigezo vya kuendesha magari ya. wanafunzi na kujiendeleza kitaaluma.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI