********************
NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
Ligi ya mpira wa miguu inayojulikana kwa jina la BIBI CUP imeanza rasmi hii leo katika uwanja wa shule ya msingi Ruzinga uliopo katika kijiji cha Rwanda kata Ibuga Tarafa kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Ligi hiyo imedhaminiwa na taasisi ya BIBI TRUST yenye makao yake makuu mjini Bukoba ikiziusisha timu zipatazo nne(4) Busingo A Busingo B, Butundu-Bunene na Kitunga-Kyamawa.
Akitoa neno la ufunguzi wa ligi Robert Rwegasira ambaye ni mratibu wa ligi hiyo amesema kuwa, lengo la ligi hiyo ni kuwaweka vijana wa kijiji cha Rwanda kuwa wamoja na pamoja na kuonyesha vipaji vyao kwenye jamii.
"Tunatambua mchango wa vijana katika kijijini chetu, hivyo tumeamua kuanzisha ligi hii ili kuwaweka pamoja vijana na kuonyesha vipaji vyao kwani kupitia ligi hii vijana wanaweza kuonekana na kujipatia ajira katika ligi mbalimbali" alisema Rwegasila.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Rwanda, Majid Ayubu ameishukuru taasisi ya BIBI TRUST kwa kuanzisha ligi hiyo huku akiwaomba viongozi wa taasisi hiyo kutambua vijana ambao wataonekana kuwa na vipaji kuwasogeza mbele kucheza hata katika virabu vya mkoa.
"Tunawashukuru viongozi wa taasisi ya BIBI TRUST kwa kuangaa ligi hii, vijana na wanakijiji tumepokea jambo hili kwa furaha ila tunaomba kuwasaidia vijana watakaoonekana kuwa na vipaji kuwasogeza mbele wakanufaike na vipaji vyao" alisema mwenyekiti Ayubu.
Waliofungua dimba ni vitongoji Busingo A na Busingo B. Matokeo: 4 - 4. Inaendelea hadi tarehe 04 Septemba 2022 atakapopatikana mshindi.
Kwa mjibu wa Taasisi ya BIBI TRUST lengo la taasisi hiyo ni kuunganisha vijana, kuleta hamasa kwa wanakijiji, kuleta burudani kwa wanakijiji na jirani zao, na kujenga afya za vijana.
0 Comments