******************
KIKUNDI cha Super Women 2017 kimetoa msaada wa vyakula kwenye kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Buloma kilichopo Mtaa wa Sofu Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo katibu wa kikundi cha Super Women 2017 Maria Msimbe alisema jamii inapaswa kusaidia makundi yenye uhitaji.
Msimbe alisema kuwa kikundi chao ambacho ni cha kusaidiana na kukopeshana fedha kinachoundwa na wanawake kimetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mapato yao.
"Fedha tulizonunulia chakula kwa ajili ya kituo hicho zinatokana na mfuko wa jamii ambao ni sehemu ya michango ya wanachama na fedha hizo hutumika kwa ajili ya matendo ya huruma kama hili,"alisema Msimbe.
Naye Mlezi wa kikundi hicho Beth Msimbe alisema kuwa misaada kama hiyo ni sadaka ambapo wanaotoa Mungu anawaongezea hivyo jamii wakiwemo watu mmoja mmoja au vikundi wasaidie makundi maalumu kwani yana changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kwenye masuala ya afya,elimu,malazi na lishe.
Kwa upande wake Msaidizi wa kituo hicho Baraka Peter alisema kuwa kituo hicho kinalea watoto wadogo ambapo kuna wanaosoma shule za msingi,sekondari,vyuo na vyuo vikuu.
Mwisho.
0 Comments