Header Ads Widget

IDADI YA WATU WALIOHESABIWA NI ASILIMIA 99.93- MTAKWIMU MKUU

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

IDADI ya watu waliohesabiwa nchi nzima katika zoezi la Sensa ya Watu na makazi lilioanza Agosti 23 Mwaka huu imefikia asilimia 99.93 ambapo imebaki  kiwango cha asilimia 0.07 ya Kaya zote nchi nzima . 


Mtakwimu Mkuu wa wa Serikali Dk.Albina Chuwa ameyasema hayo leo Jijini hapa Mtakwimu huyo alisema hatua hiyo iliyobaki itakwenda kukamilika hadi tarehe 2 2022 September na zoezi hilo litafanyika kwa njia ya simu zilizotolewa zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa .


Dkt Albina Chuwa alisema utaratibu Maalum utaandaliwa wa namna ya kuzifikia Kaya hizo kupitia Viongozi wa mitaa na vitongoji 


Kwa Upande wa sensa ya majengo ambayo ilianza jana Dkt Chuwa amesema hadi kufikia Agosti 31 mwaka huu jumla ya majengo yalikwisha hesabiwa ni Milioni 6,351,927 ambapo taarifa ya umiliki ,mahali yalipo na taarifa nyingine zilizoainishwa katika Dodoso la Majengo zimekusanywa.


" Kwa makadrio ya Oparesheni Anwani za makazi tunategemea kuhesabu majengo yapatayo Milioni 12.7 kwa nchi mzima," alisema Dkt Chuwa.


Na kuongeza" Kama tunavyofahamu  Serikali kwa Mara ya kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 sensa ya Watu na makazi ya kidigitali ambayo imejumuisha sensa ya majengo na sensa ya Anwani za makazi katika Mfumo wake wa utekekezaji.



UTOFAUTI YA SENSA YA WATU MAKAZI NA SENSA YA MAJENGO


Dkt Chuwa alieleza Sensa ya Watu na makazi hapa nchini hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya takwimu Sura 351 kifungua kidogo Cha 6(2)(a) sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 na Kama zilivyikuwa  sensa nyingine zilizokwisha  kufanyika hutumia miongozo ya Umoja wa mataifa kwa Kuwa matokeo yake yanatumika kitaifa na Kimataifa.


Hata hivyo Dkt Chuwa alibainisha sensa ya majengo Dodoso lake linamaswali 27, taarifa zinazokusanywa zinazohusu aina na sifa za Majengo,idadi ya majengo na Nyumba (unit)zilizopo ,hali ya ujenzi /ukaazi na sababu za jengo kutumika.


Alisema ubora , umiliki na jina la Mmiliki wa jengo matumizi ,upaji na uwepo wa nyaraka za kisheria za Mmiliki halikadhalika  taarifa kuhusu vifaaa vya ujenzi ikiwemo kusakafia ,kujengwa kuta na kuezekq  Pamoja na huduma nyingine zilizomo  katika jengo zinazoendelea kukusanywa nchi nzima.


"Kuhusu Bajeti ya sensa ya Watu na makazi na sensa ya Majengo inayoendelea nchi mzima kwamba Bajeti iliidhinishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 ni kiasi Cha TSHs Bilioni 400 sawa na wastani wa TSHs.6,265 au dola za kimarekani (USD) 2.7 kwa mtu mmoja," alisema Dkt Chuwa



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI