Na Gabriel Kilamlya MatukioDaimaApp ,Njombe
Serikali mkoani Njombe imesema haitarajii kuona zoezi la Sensa ya watu na makazi linaharibikia mikononi mwa makarani waliofundishwa na kula kiapo bali walitekeleze kwa viwango na kwa weledi mkubwa.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka anatoa kauli hiyo mbele ya makarani,Wasimamizi wa maudhui pamoja na wataalamu wa TEHEMA takribani 322 wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa mkoa mzima na kwamba makarani hao wanategemewa sana na taifa katika kuliendesha zoezi la kuhesabu watu na makazi hapo agosti 23 mwaka huu kwenye sensa.
Aidha anatumia fursa hiyo kuwaonya makarani watakaothubutu kutaka kuharibu zoezi hilo kwani serikali imejipanga vyema katika kuhakikisha linafanikiwa vizuri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kuluthum Sadick amesisitiza kwenda kufanyika kwa zoezi la sensa kwa ufanisi mkubwa na kwamba wanapaswa kutumia busara kubwa pindi wanapokutana na makundi tofauti ya watu kwenye kaya zao.
Boniface Hilary ni mratibu wa sensa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye anasema wamewapika makarani wote vizuri na kuwapa vifaa vya kwenda kutekeleza zoezi hilo na kwamba hawatarajii kuona kuna mmoja wapo anakwenda kinyume na maelekezo waliyopewa.
Baadhi ya Makarani hao akiwemo Joshua Mbilinyi,Julia Mtanga na James Mapunda ambaye ni mtaalamu wa TEHEMA wanakiri kuwa elimu walioipata watakwenda kuifanyiakazi kikamilifu kama matarajio ya serikali yalivyo.
Mafunzo kwa makarani hao yamefungwa kwa nchi nzima baada ya kusoma kwa zaidi ya siku 18 ambapo Agosti 23 mwaka huu zoezi la sensa linaanza ramsi.










0 Comments