Header Ads Widget

BODI TPDC YAVUTIWA NA MIKAKATI YA UTAFITI NA UCHIMBAJI WA GESI INAYOENDELEA MTWARA

  


Na Matukio DaimaAPP, Mtwara

Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania 

(TPDC) imevutiwa na mikakati ya iliyopo ya kuongeza kasi ya tafiti nchini za uchimbaji wa gesi katika maeneo mbalimbali ndani ya bahari na nchi kavu hatua ambayo itaiweka nchi katika hali nzuri kiuchumi na kimazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa bodi hiyo Balozi Ombeni sefue  alisema kuwa taasisi hiyo imejipanga kuongeza uzalishaji wa gesi nchini hivyo kujikita katika tafiti.

 

“Hii bodi ni mpya ilikuwa muhimu kufika na kuona kazi zinazofanyika ili kuweza tumeona kazi kubwa inayofanywa katika tafiti na pia yapo maeneo bado tafiti zinaendelea ili tuweze kutekeleza vyema shughuli hii tuliyokabidhiwa na serikali” 




Kwa upande wake Dr Natu Mwamba Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi TPDC  alisema kuwa usimamizi mzuri na uendelezaji katika sekta ya gesi utaleta manufaa kwa nchi.


“Nimeona visima vya gesi katika maeneo mbalimbali hii inaonyesha kwa watalaamu wetu wako tayari kuongeza uzalishaji wa gesi ndio maana tumeona visima vilivyofanyiwa utafiti tayari lakini ameona tafiti zikiendelea jambo ambalo linatia moyo kwa nchi” aliema Dr Mwamba


Kwa upnade wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania 

(TPDC)  Dr James Mataragio  alisema kuwa ugunduzi umefanyika tupo katika hatua za kuendeleza eneo miezi 18 ijayo gesi itaanza kuzalishwa toka futi za ujazo 60 hadi 140 kwa siku.


Alisema kuwa kuwa kwasasa wapo katika  mazungumzo namna ya kujenga bomba na kupeleka katika kiwanda cha kuchakata gesi Madimba ambapo litakuwa na urefu wa mita 35”


“Tunataka kuongeza uzalishaji hadi kufikia futi za ujazo 140 kutokea 60  kwa sasa Mazingira ni mazuri bei ya mafuta imepanda na wawekezaji wengi wamejitokeza nchini tunategemea kuwa na wawekezaji wengi kwenye sekta ya gesi”  alisema Mataragio 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI