Header Ads Widget

ZAIDI YA WANANCHI 11,000 KUPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA.

 




Na Bahati Sonda, Bariadi.



Zaidi ya wananchi 11,000 wa vijiji vya Sengerema, Majengo, Mwamondi pamoja na Mtaa 1 wa Mwakibuga vilivyopo katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wanatarajia kuondokana na kero kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama waliyokuwa wakikabiliana nayo kwa muda mrefu  hali iliyowalazimu kuchota maji katika visima vifupi sambamba na malambo.


Wananchi hao wanaondokana na kero hiyo kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa maji wa Sengerema katika halimashauri ya wilaya ya Bariadi ambao utasaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika vijiji hivyo.


Hayo yamebainishwa mapema jana na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Mhandisi Mapengu Gendai wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2022 Sahili Nyanzabara na kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kutoka 35% iliyopo sasa mpaka 88.5% baada ya mradi huo kukamilika.


Aidha Mhandisi Gendai amebainisha kuwa chanzo cha mradi huo ni kisima kirefu kilichopo katika Kijiji hicho cha Sengerema chenye uwezo wa kuzalisha maji lita za ujazo 320,000 kwa siku hivyo kuweza kukidhi mahitaji ya vijiji hivyo na kwamba umegharimu  kiasi cha shilingi bilioni 1.06 .


Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2022 Sahili Nyanzabara ameyataka makampuni na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo kuteleza kwa kiwango na ubora wa hali ya juu huku akiwataka viongozi wa taasisi zenye miradi mbalimbali kusimamia vizuri katika kila hatua ili ilete matokeo mazuri kwa wananchi.


Hata hivyo katika hatua nyingine Nyanzabara amewataka wananchi kuvuta maji kwenye familia zao ili waweze kunufaika na miradi hiyo ya serikali inayotekelezwa na Ruwasa hivyo kuweza kufikia dhana halisi ya kumtua mama ndoo kichwani.


Awali wakizungumzia mradi huo wa maji wananchi wa vijiji hivyo akiwemo Tabu Nyanda wamesema kuwa walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji kwa muda mrefu huku wakichangia maji na mifugo hali iliyokuwa ikipelekea kuwalazimu kutumia maji ambayo si safi na salama ambapo pia ilipelekea kusimama kwa shughuli  za uzalishaji na  kukiri kuwa mradi huo utakuwa ni mkombozi kwao.


 " Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2022"Sensa ni msingi wa maendeleo , shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo yetu" .

              


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI