Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es salaam
Taasisi ya Yuhoma Education Limited inayojishughulisha na utoaji wa ushauri kwa wanafunzi wanataka kusoma nje ya nchi wameiyomba Serikali iwasaidie kukutanishwa na Balozi mbalimbali zilizopo Tanzania Ili kuondoa ukiritimba kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nje.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo, Yusuph Yahaya wakati alipokua akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 17 ya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia ya yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja.
Amesema kuwa wamekua wakikutana na changamoto mbalimbali katika kuwasaidia wanafunzi kusoma nje ya nchi ikiwemo kupata passport kwa wakati pamoja na wazazi kuwa na uwelewa mdogo tangu ilipotokea ugonjwa wa Corona pamoja na vita vya Ukraine ambapo wamekua na wasiwasi kusafirisha watoto wao.
Ameongeza "Ili mwanafunzi apate passport lazima awe na NIDA, lakini anapofika uhamiaji kunakuwa na changamoto kwani namba ya NIDA inachukua muda kupatikana mzunguko wake unakua mrefu"
"Kwenye jambo zuri siku zote lazima kuwe na kasoro, tunaipongeza Serikali kupitia tume ya vyuo vikuu TCU kwa kuandaa maonesho haya kwani yamekua na tija sana wazazi na wanafunzi wanafika hapa na kujionea mabanda mbalimbali na kuchagua vyuo wanavovitaka, zamani hayakua makubwa kwa namna hii"amesema Yusuph.
Amesema kuwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaeka katika mazingira mazuri Ili tuende Tanzania waweze kuwa na nafasi kubwa ya kuweza kupata
"Tunaomba Serikali itusaidie kupata Mawasiliano makubwa na Tume ya vyuo vikuu TCU na Wizara ya elimu kutupatia Mawasiliano ya kuona na Balozi zilizopo nchini kwani kuna kuwa na mlolongo mkubwa mpaka kuna muda tunahisi hatuhitajiki kutokana na mambo ya kidiplomasia"amesema Yusuph.
Aidha, amesema taasisi hiyo inahusika na kutoa ushauri wa kielimu kwa wanafunzi wanaohitaji kusoma nje ya nchi na kuwashauri kozi gani gani wasome Ili kuendana na Soko la ajira ndani na nje ya nchi Ili kuondokana na mawazo ya kuajiriwa.
"Tumegundua tuna kila sababu ya kuwashauri wanafunzi kuweza kusoma nje na kozi ambazo zitawasidia kuingia kwenye ushindani wa Soko la ajira, tunawashauri wakasome wapi na wakasomee nini na wapi"amesema Yahaya.
Amesema kuwa, yeye kama mdau wa elimu anatamani aone wanafunzi wanapewa ushauri kusoma kozi gani ambazo zinahitajika ndani na nje au duniani Ili waondoe msongamano wa watu wanaohitaji ajira Serikalini.
Aidha, ameongeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa maonesho amewataka mawakala wa vyuo vikuu kuchagua wanafunzi wanaoendana na Soko la ajira.
0 Comments