Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa taasisi binafsi zinazosaidia kutoa elimu juu ya kujikwamua kiuchumi ili kusaidia wananchi kukuza mitaji na kuleta maendeleo kuanzajia ngazi ya familia Hadi Taifa.
Hayo yalisemwa na naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu Ajira,vijana na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi katika kongamano la miaka siku ya taasisi inayoshughilika na kutoa elimu ya kuweka na kukoka YEMCO - VICOBA jijin Dar es salaam.
Katambi amesema kwa namna taasisi hiyo inavyoonesha njia kwa makundi mbalimbali na kusaidia wananchi kujikwamu kiuchumi kwa kutumia njia ya -VICOBA endelevu
"Mkurugenzi wa YEMCO VICOBA unamaono mazuri,na mchapakazi unayejitambua kwa juhudi hizi zinazoonekqna kwa kusaidia makundi haya serikali itatengeneza mazingira wezeshi ya kuhakikisha unasonga mbele ili kuikomboa jamii katika wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi".Alisema Katambi
Pia alisema vijana hawana budi kuiga mfano wa Bananga kwa kila halmashauri ili kuwasadia wananchi katika maeneo hayo tuwasaidie vijana ili kuunga serikali mkono kwa kunufaika na makusanyo yanayopatika katika
Kila halmashauri asilimia 10."Alisema Katambi
Kwa upande wake naibu waziri wa habari ,mawasiliano na Teknolojia mheshimiwa Kundo Methew ambaye pia ameshirikia katika kongamano Hilo Alisema pamoja na kukuza uvhumi kupitia bidhaa mbalimbali ni lazima wajasiliamali.hao kutumia Teknolojia ya mawasiliano kuuza bidhaa zao nje ya nje.
Bidhaa zenu ni nzuri lazima zibuke mipala nje ya nchi,hapa Tanzania Kuna vicoba vingi Sana lakini tunaomba tuvuke kupitia mwamvuli mmoja mbao ni YEMCO-VICOBA.alisema mheshimiwa Kundo
Pia aliongea serikali kuweza kutumia fursa ya kutafuta masomo nje ya nchi itakuwa rahisi namna ya kuratibu zoezi Hilo na yeye ambaye ni msimamiz wa Wizara ya mawasiliano na Teknolojia atahakikisha taasisi hyo inajulikan zaidi kwa kutumia matangazo mbalimbali,Alisema waziri Kundo.
Pia katika suala la mifumo ya kusajiriwa kwa kutumia tehama litashughulikwa haraka ili kurahisisha huduma hiyo kwa wananchi kwanj serikali kwa Sasa inapunguza changamoto ya wananchi kutoka sehemu moja Hadi nyingine kufuatia huduma ya kusajiriwa biashara hivyo zoezi Hilo linafanyika kwa mtandaoni hivyo litaendelea kuboresha palipo na changamoto.
Mkurugenzi wa taasisi inayoshughilika na kutoa elimu ya kujikwamu kiuchumi kuweka na kukopa ambaye pia ni Rais wa Vicoba Mohamed Basanga alibainisha mafanikio mbalimbali walioyopata tangu kuanzishwa taasisi hyo ni pamoja kuwaunganisha wananchi kutoka sekta mbalimbali kupata elimu ya kujikwamua kiuchumi na Sasa wamefika hatua ya kumiliki usafiri wa Kosta ambayo imezinduliwa na waziri Katambi.
YEMCO -VICOBA tumeweza kuunganisha vikundi kutoka katika sekta ya wasanii,walimu,wasafirishaji wa bajajinna bodaboda,wajane,vyama vya siasa kila kata na kwasasa wameanza na kwa Sasa wanatajia kuwa na kufungua vituo katika wilaya mbalimbali hapa nchini ili kutoa elimu ya Vicoba na kutumia fursa zinazowazunguka,Alisema Bananga
Pia alielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili ni pamoja na kucheleweshewa vibali vya kufanya kazi katika wilaya na kurudisha nyuma Ari kwa wananchi kujiunga na vikundi ili kujikwambua kiuchumi.
"Tunapewa vibali vya kufanya kazi na mkurugenzi lakinintunapogika katika kata mtendaji wa kata hakikibali mpaka tuombe Tena kibali kinachoainisha kata yake hili linatuchelwesha kufanya kazi."Alisema Bananga
Pia aliongea changamoto nyingine ni usajiri wa vikundi kwa njia ya mtandao tunapotuma Taarifa ya kikundi kwenye mtandao inakaa mida mrefu bila kupata majibu na hakuna ,baadhi ya vikundi wanayuona sisi tunawatapeli maana mfumo hauletirejesho tunaomba hili liangaliwe ili kurahisisha usajiri kwa wanavikundi na kuchochoa maendeleo kwa.wananchi.Alisema Bananga.
Katika kongamano Hilo mwezeshaji wa mafunzo ya kukuza biashara kutoka YEMCO-VICOBA Charles Nduku alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wajasiriamali kuheshimu wateja na kuendelea kuboresha bidhaa zao kwa kufuata kanuni bila libadilisha radha za bidhaa zao kwa wateja.
"Mteja anahitaji kumuona muuzaji wa bidhaa anamuonekano mzuri,usafi na lugha nzuri ya biashara tusilalamike.kiwa hakuna wateja wakati wewe mwenyewe huna lugha nzuri kwa wateja wako ,Alisema NdukuMwisho
0 Comments