Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Nishati January Makamba amesema kuwa serikali inatarajia uendeshaji wa shirika la maendeleo la Petroli nchini( TPDC) utakuwa wa ufanisi na kiwango katika kufikia mageuzi ya sekta ya gesi na mafuta nchini.
Makamba amesema hayo leo wakati akizindua bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo jijini Arusha na kueleza kwamba uteuzi wa bodi hiyo unaakisi dira na Malengo mapya ya serikali .
Makamba aliitaka bodi hiyo kuhakikisha wanayafikia maendeleo ya nchi, Dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa Gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.
"Dhamira yetu ni kuona shirika hili linatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu bali uendeshaji wa rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi" Alisema Makamba
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni katibu mkuu Kiongozi mstaafu amesema wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda inavyotakiwa na sekta hii ili taifa liweze kunufaika na rasilimali zake za mafuta na Gesi tulizopewa na Mungu.
Mikakati iliyopo kwa sasa ni ile ya serikali na haijaanza leo tutaipitia kama bodi mpya tumefanikiwa wapi na changamoto ni zipi na zitatatuliwaje ili kazi iendelee vizuri kujenga TPDC yenye kusaidia serikali.
Awali Mkurugenzi wa Shirika la mafuta na Gesi nchi mhandisi ,James Maragio amesema kuwa miradi ya mafuta na Gesi itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi.
Hatahivyo,mkurugenzi wa shirika la udhibiti la petroli nchini,Mhandishi Charles Sangweni alisema kuwa wao kama wadhibiti wanatarajia makubwa kupitia bodi hiyo kwa kuwa hapo awali shughuli nyingi hususani maamuzi yalikwama kutokana na kutokuwepo kwa bodi hiyo.
0 Comments