Na Gabriel Kilamlya , MATUKIODAIMAAPP,NJOMBE
Jumla ya wananchi 93729 wanatarajiwa kufikiwa katika kampeni maalumu ya utoaji chanjo ya Covid 19 awamu ya tatu inayoendelea mkoani Njombe ili kukabiliana na wimbi la ugonjwa wa Corona ulioyakumba mataifa mbalimbali duniani.
Kampeni hii maalum inafanyika kwa muda wa siku Nane kuanzia tarehe 11 hadi 18 mwezi huu.
Mbele ya vyombo vya habari mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba anatoa ripoti hiyo na kwamba hivi sasa kiwango cha zoezi la uchanjaji kimepanda maradufu kutokana na kazi kubwa inayofanywa na wakuu wa wilaya kupitia mikutano yao ya hadhara pamoja na wasanii wanaohamasisha.
Mratibu wa chanjo mkoa wa Njombe Linda Chatila anasema chanjo hiyo kwa awamu hii itatolewa nyumba kwa nyumba na katika makusanyiko mbalimbali.
Pia Chatila anawatoa hofu wananchi juu ya chanjo hiyo.
Baadhi ya wakazi mkoani Njombe akiwemo Syrivia Kibunda na Paternus Mgungilwa wanasema awali walikuwa na hofu juu ya Chanjo hiyo lakini hivi sasa wamepatiwa elimu ya kutosha iliyowafanya kujitokeza kuchanja.
''Njombe ina chanja,Ujanja ni kuchanja'' ni Kauli mbiu inayotumika katika zoezi hili Mkoani Njombe.
0 Comments