Header Ads Widget

WANAMICHEZO WANAOSHIRIKI UMITASHUMITA WATAKIWA KUONESHA VIPAJI VYAO VITAKAVYOFANYA MKOA WA MWANZA KUIBUKA KIDEDEA

 


NA CHAUSIKU SAID ,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA 

Wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya umitashumita Mkoani Mwanza wametakiwa kuhakikisha wanaonesha vipaji vyao vitakavyosaidia halmashauri ya jiji kuwa washindi na kuwakilisha Mkoa huo vizuri.

Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Msingi Jiji la Mwanza Mussa Lambwe wakati akifungua umitashumita kwa wanafunzi wa shule ya misingi na kuwataka kucheza kwa bidii ili kuendela kuwa washindi kwa mwaka mwingine


Lambwe amesema kuwa Mkoa wa Mwanza umekuwa ukiogopwa na Mikoa Mingine katika mashindano hayo kwa kuwa wamekuwa na wachezaji wazuri wanaoshiriki michezo hiyo ipasavyo nakupelekea kuwa washindi kila wakati.

"Ninapotazama kwenye sura zenu na muonekano wenu ninaona vipaji,  hata nilipofika hapa nimekaribishwa na vipaji nikasema niko mahali sahihi" Alisema Lambwe

Amefafanua kuwa halmashauri ya jiji la Mwanza imekuwa ikoongoza kwa halmashauri zote Tanzania nzima hivyo atashangaa kuona mwaka huu katika michezo hiyo watapatikana wachezaji ambao hawataweza kuiwakilisha vyema katika mashindano.

" natarajia kuona wale ambao wanajua kucheza na sio wanaocheza rafu na watakaosababisha tufungwe" Alisema Lambwe.

Agnes Majinge ni Afisa utamaduni Jiji la Mwanza amesema kuwa wamezindua rasmi mashindano hayo ya umitashumita Ngazi ya Wilaya kwa ajili ya kutengeneza timu ya wilaya, pamoja na kuhaikisha kuwa mwaka huu wanakuwa na timu bora itakayowakilisha wilaya ya Nyamagana.

Majinge amesema kwa kuwa michezo ni ajila watahakikisha wanaangalia vipaji vitakavyosaidia kutengeneza timu katika mashindano ya Mkoa.

" Tutahakikisha tunalea vipaji vya haea watoto ili waweze kufika ngazi ya taifa na wale amabo wataonesha vipaji na kuchaguliwa tutasimama nao" Alisema Majinge.

Kwa upande wake Afisa Michezo Jiji Mohamed Bitegeko amesema kuwa mashindano hayo ya umitashumita kuna kanda nne ambazo zitaunda timu ya halmashauri ya jiji la Mwanza

Bitegeko amesema kuwa timu zitakazocheza ni kata zote 18 za halmashauri ya jiji la mwanza ili kuweza kuchagua watakaishiriki watakaocheza Mkoa.

Aidha ametaja baadhi ya michezo itakayochezwa katika mashindano hayo ya umitashumita ni pamoja na mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa pete kwa wanawake, pamoja na michezo ya watu wasioona.

Bitegeko amefafanua kuwa katika zoezi la kuchagua wachezaji bora watashirikiana kwa karibu na vyama vya michezo ili kuondoa malalamiko pamoja na kupata timu iliyo bora.

Angel Waziri,  Rahel Mashiku Ni baadhi ya washiriki katika michezo hiyo wamesema kuwa michezo inafaida nyingi katika mwili itawasaidia miili yao kuwa imara lakini pia michezo ni ajira kama ajira zingine.

" watu wengi husema mtoto akicheza anapungukiwa na kazi lakini jambo hilo ni la uongo" Walisema











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI