Header Ads Widget

TRC YASAINI MKATABA WA KUKARABATI MABEHEWA NA USHOROBA WA KATI

 




Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam


Shirika la TRC limetiliana saini ya makubaliano ya Mkataba na Ushoroba wa kati wa Ukarabati wa Mabehewa ya Mizigo ya Zamani 20 ili kuongeza ufanisi na uwezo wa Shirika katika ubebaji mizigo.


Akizungumza katika hafla hiyo ya utoaji saini Mkurugenzi wa Shirika La Reli Mhandisi Masanja Kadogosa amesema Mkataba huo umegharimu zaidi ya Bilioni Moja, ambapo lengo la mradi huo ni kuipa uwezo TRC katika usafirishaji wa mizigo.


"Lengo la mradi huo ni kuipa uwezo TRC katika usafirishaji wa mizigo kwa kutumia reli ya MGR ambapo makubaliano hayo yatachukuwa Muda wa miezi 24 yakihusisha ununuzi wa vipuli kwaajili ukarabati wa mabehewa haya"amesema Mhandisi Kadogosa.


Ameongeza kuwa, behewa hizo pia zitasaidia kusafirisha mizigo ya wateja wa nchi jirani za Uganda, DRC, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini kwani hivi karibuni Shirika limeingia Mkataba na Kampuni ya Roofing kutoka Uganda kusafirisha mizigo yao ambapo TRC itatoa behewa 20 na Shirika la Reli Uganda – URC litatoa behewa 60 kwaajili ya kazi hiyo.



Kwa upande wake,  Katibu Mkuu wa Ushoroba wa Kati Okandju Okonge amesema kutoa fedha hizo ni kusaidia kuongeza Mabehewa kwani kumekuwa na Uhitaji mkubwa katika Usafirishaji wa Mizigo kwenda kwenye Nchi zilizopo kwenye Ushoroba wa kati.


Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli la Tanzania Prof. John Kindoro ametoa wito kwa wadau mbalimbali na Sekta Binafsi kujitokeza katika kuisaidia TRC katika Kukarabati Mabehewa Hayo ya Reli ya Zamani ili kufufua Reli hiyo na kupunguza Matumizi ya Barabara ambayo yanagharama kubwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS