Header Ads Widget

TAMASHA LA UTAMADUNI LATAMATISHWA DAR,

 


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamed Mchengerwa amesema Tamasha la utamaduni litakua endelevu ambapo amewataka viongozi wa Mila kuendelea kukemea vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya mtanzania.


Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga tamasha la kwanza la  kitaifa la utamaduni katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam liloanza Julia 1 hadi 3.



Aidha, amesema kuwa licha ya kuwa tamshasha hilo limefanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania lakini limefanikiwa kutazamwa na watu mill 10 kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ambapo Serikali inakwenda  kutengeneza studio kila wilaya kwa ajili ya kurekodia kazi za sanaa.


Amesema kuwa, wizara imejipanga vizuri kuhakikisha Tamasha la kitaifa la pili la Utamaduni litakalofanyika mwakani litakuwa katika kiwango cha kimataifa.


Aidha amesema wizara yake inakwenda  kutekeleza maelekezo ya viongozi wetu ya kuthamini, kuandaa  mavazi ya taifa ili kuhakikisha mila na desturi za mtanzania zinaendelezwa.


"Ni matarajio yangu kuwa mikoa yote itakaoanza sisi kama wizara tutakuja mara moja,tunahitaji watanzania wakae katika furaha katika maisha yao" amefafanua  Mchengerwa.



Kwa upande mwingine Selikali imeanzisha Mfuko wa Utamaduni kwa lengo la kuwasaidi wasanii nchini ambapo amesema tayari kwa mwaka 2022/2023 umetengewa shilingi bilioni mbili kwa kazi hiyo.


Katika tamasha  hilo pia  amekabidhi zawadi kwa washindi wa ngoma na vyakula  vya asili ambapo washindi wa ngoma za asili ni mkoa wa Mwanza ambao umekuwa namba moja, Lindi ambao umekuwa namba mbili na mkoa wa Mjini magharibi  umekuwa wa tatu.






Kwa upande wa vyakula vya asili mkoa Kilimanjaro umeongoza ukifuatiwa na mkoa wa Tanga na Kagera ikishika namba tatu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI