Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleimani Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.
Chegeni aliteuliwa July 28,2022 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Ally Hapi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Uapisho utafanyika Ikulu Dar es salaam Agosti 01,2022.
0 Comments