**************************
Amon Mtega, Mbinga.
UCHAGUZI wa Viongozi wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi CCM katika ngazi za kata kwenye Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma zimepamba moto kutokana na hamasa ya Viongozi wa CCM Wilayani humo na wajumuiya zake.
Katika uchaguzi huo Jumuiya ya Wanawake UWT ndiyo iliyoanza kwenye kata zote 48 za Wilayani humo za kuwapata Mwenyekiti ,Katibu pamoja na mjumbe wa Halmashauri kuu ambapo kwa kata ya Mbinga, A, ya mjini Mbinga katibu aliyeibuka mshindi ni Notburga Kapinga ambaye ameibuka na kura 15 huku mwenyekiti wake Mariana Ngaleka ambaye ameibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Hosana Ndunguru.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo Alex Andoya amesema kuwa wapiga kura (Wajumbe) walikuwa 15 na kuwa katibu huyo kashinda kwa kura zote 15 huku mpinzani wake Anna Mlelwa hakiweza kupata kura.
Msimamizi Andoya amesema kuwa taratibu zote zimefuatwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi na kuwafanya wagombea wote wameridhika kufuatia uchaguzi huo.
Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya UWT ngazi ya kata Notburga Kapinga amewashukuru Wajumbe hao kwa kumpa dhamana hiyo na kuwa atafanya kazi ya Jumuiya na Chama cha Mapinduzi CCM kwa kushirikiana nao.
Naye katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Jacob Siayi akiwa ofisini kwake amesema kuwa chama na Jumuiya zake kimejipanga vema na sasa umeanza uchaguzi ngazi za Jumuiya ambapo Jumuiya ya Wanawake UWT ndiyo imeanza katika ngazi za kata.
0 Comments