Header Ads Widget

MKE WA MREMA AFICHUA SIRI YA MUMEWE

 


Doreen Kimbi mke wa Mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema amefichua kuwa siri ya mumewe kuendelea kupendeza kiasi cha kuanza kuwa kijana ni kumtunza na  kumuhudumia vizuri ikiwemo kuzingatia mlo kamili.


 Hayo amebainisha leo Alhamisi Juni 14, 2022 baada ya kumsindikiza mumewe Mrema kwenda kuwasilisha maoni yake Kwenye kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, Doreen amesema mtu yeyote akipewa mahitaji yake lazima atapendeza.


"Mme wangu anapendeza na kuonekana kama kijana wa miaka 20, ni kwa sababu namtunza vizuri na kumuhudumia vile inavyotakiwa ikiwemo kuzingatia mlo kamili na kwa wakati," amesema


Doreen aliyeonekana mwenye furaha wakati wote amehitimisha kwa kutoa rai kwa wanawake wenzake akiwataka  kujali ndoa zao kwa kuwapa upendo kwa kuwatunza na kuwajali wanaume wao.


Hata hivyo, Mrema mbali na kuzungumzia mambo mengine ametumia fursa hiyo kumtambulisha mkewe kwa waandishi wa Dar es Salaam huku akisema tangu kufunga ndoa hajawai kuja kumtambulisha


"Mnataka niwatambulishe mke wangu, Naibu Waziri Mkuu Msaidizi ni huyo mwanzoni alikuwa anaitwa Kimbi sahizi Mrema ni Naibu Waziri Mkuu Msaidizi wangu," amesema Agustino


Awali, wawili hao waliwasili Ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam sehemu ambayo wajumbe wa kikosi kazi wanaratibu ukusanyaji maoni kuanzia Saa 2:30 Asubuhi wakiwa Kwenye gari aina ya Harrier huku Mkewe Doreen akiendesha gari hiyo.


Mrema na Kimbi walifunga ndoa Machi 24, 2022 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboi, Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI