Header Ads Widget

MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA KUJENGA GATI BANDARI YA SAADANI

 


NA IBRAHIM KUNOGA , MATUKIODAIMAAPP,BAGAMOYO.

Mamlaka ya Bandari Tanzania imeamua kuirasimisha Bandari ndogo ya Saadani iliyopo katika Kijiji cha Saadani kata ya Mkange katika Halmshauri ya Chalinze kwa kujenga Gati itakayoipa uwezo bandari hiyo kutia nanga meli za mizigo na abiria,

Uamuzi huo umefikiwa  kwenye  kikao kilichofanyika katika kijiji hicho kati ya Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ,Mamlaka ya Hifadhi ya wanyama pori ya Saadani, Uongozi wa Halmashauri ya Chalinze na wafanyabiashara katika kijiji cha Saadani.


Akizungumza katika kikao hicho Afisa Mkuu wa Operesheni, Bwana Colman Moshi kwa niaba ya Mamlaka ya Bandari Tanzania amewahakikishia washiriki wa kikao hicho kwamba ujenzi wa Gati hiyo utaanza mara moja baada ya kuwa utafiti umefanyika na kubaini ipi ni sehemu sahihi kwa kujenga Gati hiyo,na kusema kuwa   utafiti huo kwa mujibu wa mtaalamu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania utafanyika ndani ya siku kumi na nne (14) ,baada ya hapo ripoti itawasilishwa kwa Mamlaka na utekelezaji unaanza maramoja.



Utekelezaji wa mradi huu wa Gati ni maombi ya Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete(MB) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu ili kuboresha biashara ya utalii katika Hifadhi ya Saadani na kuongeza mapato ya serikali na kukuza uchumi wa Saadani na wanachalinze kwa ujumla ,

kwani baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Gati la Saadani itarahisisha ufikaji wa watalii kwa urahisi kutoka Zanzibar moja kwa moja hadi Saadani bila kupita Dar es salaam na kwa muda mfupi,kwani umbali kutoka Zanzibar hadi Saadani ni umbali wa kilomita 45.


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze,Bwana Ramadhani Possi kwa niaba ya uongozi wa  Halmashauri ameushukuru Uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kukubali ombi la Mheshimiwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi lakini pia kuvutia utalii katika halmashauri ya Chalinze na kuongeza mapato ya serikali kuu na Halmashauri.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI