Header Ads Widget

DKT MCHEPANGE ATAKA WATU WENYE ULEMAVU KUPEWA KIPAUMBELE CHANJO YA HOMA YA INI

Na Matukio daima media,  Mbeya

IMEELEZWA kuwa watu wenye ulemavu wanaonekana kusahaulika katika jamii kwenye  masuala muhimu ikiwemo afya, elimu na mambo mengine ya msingi hivyo kundi hilo kuwa  hatarishi kwa  magonjwa ya kuambukiza. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo katika eneo la maegesho la hospitali hiyo  Mkuu wa huduma za Tiba na uongozi uchunguzi, Dkt. Uwesu Mchepange wakati wa maadhimisho ya siku ya Homa Ini Duniani, amesema kuwa kundi la watu wenye ulemavu lipo kwenye hatari kubwa ya kuambukiza homa ya Ini.


Dkt. Mchepange amesema kuwa katika maadhimisho hayo wameona vema  kulenga kundi la watu wenye ulemavu kwasababu kundi hilo limesahaulika kwenye jamii katika mambo mbalimbali ya msingi. 



Hata hivyo amesema kuwa kundi hilo lipo kwenye hatari kubwa kwenye magonjwa ya kuambukiza kwani baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia kundi la watu wenye ulemavu katika faida ili kufanya mambo yao ambayo yanaweza kulifanya kundi hilo kupata magonjwa ya kuambukiza. 


Aidha amesema katika takwimu za mwaka 2021 zaidi ya watu mil.1 wanapoteza maisha  kila mwaka kutokana na homa ya Ini duniani au vitu ambavyo vinavyoambatana na homa ya ini kwa maana madhara mbali mbali yanayotokana na homa ya Ini .


Amesema kuwa inakadiriwa asilimia 4.4 ya watanzania wanaambukizi ya virusi vya  homa ya Ini lakini mbaya zaidi watu wamekuwa wakiogopa virusi vya ukimwi kuliko virusi vya homa ya Ini wakati virusi vya homa ya Ini ni hatari zaidi kuliko ukimwi hatari yake inatokana na kwamba uwezo wa kuambukiza virusi vya homa ya Ini mkubwa zaidi kuliko virusi vya ukimwi ndo sababu ya kuliona kundi hili watu wenye ulemavu kulipa kipaumbele katika maadhimisho haya.


"Na unapozungumzia homa ya Ini hasa hii inayosabishwa na virusi hii inaambukiza kwa njia mbalimbali ambapo njia kuu  ni zile zile ambazo zinaambukiza virusi vya ukimwi" amesema Dkt. Mchepange. 


Akifafanua zaidi Mkuu wa huduma za uchunguzi hospitali ya Rufaa ya kanda  ya Mbeya amesema kuwa njia za maambukizi kuu ni  ngono  zembe haina kinga  yeyote,maambukizi  ya mama  kwenda kwa mtoto,kupitia damu  ambayo  ni sindano  kwa  wale wanaojidunga  kwenye  madawa  ya kulevya  na kwamba hizo njia kuu.


Hata hivyo Dkt. Mchepange amesema kuwa ndo sababu kuu walioona kuwa kundi la watu wenye ulemavu limekuwa likiachwa  nyuma  kwenye  mambo  mengi lakini  pia  lipo kwenye  hatari ya kupata  maambukizi ya homa ya Ini hivyo wakaona upo muhimu wa kulisaidia kundi hilo watu wenye ulemavu kupata elimu ,upimaji na chanjo  ya homa ya Ini kwa walemavu .


 Dkt.Peter Kishimbo  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani amesema kuwa magonjwa ya homa ya Ini yanaambukizwa kwa ngono zembe ,njia ya damu ,kwa mama kwenda kwa mtoto ,vitu vyenye ncha kali  na kwamba dalili za homa ya Ini njano kwenye macho ,homa,tumbo kuuma upande wa kulia, viungo kuuma ,kuharisha na kutapika.


“Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Mbeya ,Juma Mwampepo amesema kuwa wanashukuru hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kwa kutambua umuhimu wa kundi la watu wenye ulemavu ili kupata elimu ya homa ya Ini kwasababu wengi wao walikuwa hawaifahamu hivyo wamefumbuliwa macho na kupata somo kubwa.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI