Header Ads Widget

BOSS MASOKO VUNJA BEI ACHUKUA FOMU UENYEKITI WAZAZI CCM MKOA WA IRINGA

 


MKURUGENZI wa Masoko wa kampuni ya Vunjabei Ltd, Fadhili Ngajiro amechukua fomu kugombea Uenyekiti wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi,  Mkoa wa Iringa.


Ngajiro aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Iringa kati ya mwaka 2008  na 2012 alichukua fomu hiyo leo katika ofisi ya CCM ya mkoa.

Katika mchakato wa ndani wa chama hicho kutafuta nafasi ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa Mjini mwaka 2020 alishika nafasi ya tatu kati ya wagombea 52 waliojitokeza.

"Mimi ni mwanachama wa CCM na wa Jumuiya ya Wazazi,  nimechukua fomu kuwania nafasi hiyo nikitekeleza haki yangu ya msingi ya kikatiba” alisema kwa kifupi baada ya waandishi wa habari kumzonga kwa maswali wakati akitoka kuchukua fomu hiyo.

Wengine walioonekana katika ofisi hizo za CCM Mkoa ni pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa,  Salim Asas,  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa,  Dk Abel Nyamahanga na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Albert Chalamila.

Pamoja na watatu hao kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi,  walikataa kuzungumza na wanahabari kueleza nafasi wanazowania.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI