UMLA ya Tani 3921.14 za ufuta wa chama kikuu cha ushirika Lindi mwambao zimeuzwa kwenye mnada wa kwanza wa chama hiko ambapo bei ya juu ilikuwa 3025 na bei ya chini 3015 .MWANDISHI HADIJA OMARY MATUKIODAIMAAPP, LINDI
Mnada huo umefanyika jana kwenye chama cha msingi pachani AMCOS kijiji cha mipango wilayani lindi ambapo jumla ya makampuni 28 yalijitokeza kuomba kununua ufuta .
Meneja wa chama cha kikuu cha ushirika Lindi mwambao Saidi Swalehe amesema ufuta huo uliouzwa ni kutoka kwenye maghala makuu manne ambayo ni Tanroad Nangurukuru,Buko Lindi,Hazina na Ilulu-mtama.
Nae mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amewasisitiza wanunuzi kufanya malipo kwa wakati kwa wakulima kulingana na taratibu zilivyowekwa.
Kwa upande wake mrajisi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi Cesilia costenes aliwataka wakulima wa zao hilo kutumia fedha watakazozipata kutoka kwenye mauzo hayo kuzitumia kwenye mambo ya maendeleo
Nae Mwanahamisi Bakari Mkulima Mkazi wa mipingo aliishukuru serikali kwa kusimamia vyema uuzaji wa zao hilo ambao unaleta tija kwa wakulima kwa kupata bei Mzuri









0 Comments