Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
VIONGOZI wa Vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wameahidi kutoa mikataba ya kazi kwa Madereva ikiwa ni pamojana kuzingatia rasimu ya mkataba ya ajira ulioandaliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau.
Mnamo tarehe 24 Aprili,2022 serikali ilikutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Madereva kwa lengo la kusikikiza hoja ,kero na malalamiko yaliyowakabili katika uendeshaji wa shughuli zao za usafirishaji wa mizigo na abiria nchini.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini hapa Naibu Waziri wa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Ajira,Vijana na wenye Ulemavu Patrobas Katambi amesema serikali imezifanyia uchambuzi hoja zilizowasilishwa pande zote na kuona kunahaja ya Kuendelea na zoezi la kufanya ukaguzi jumuishi za wadau wanaoguswa na sekta ya usafirishaji.
"Kaguzi hizi zimeanza kufanyika katika Mikoa ya Dar es slaam na zinaendelea katika mikoa mingine yote hapa nchini na zoezi hili litakamilika ifikapo mwezi Agosti ,2022," alisema Katambi.
Aidha alisema kuhusu mishahara ya Madereva kupitia benki,wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wapo tayari kutekeleza jambo hilo ambapo amesema kwa kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini imeruhusu mwajiri na mfanyakazi kukubaliana namna ya kulipana mshahara kupitia benki fedha taslim au hundi.
Alisema kuhusu Bima ya Afya NSSF na Pensheni kwa wastaafu wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wameahidi kuzingatia matakwa ya sheria kwa kuwasajili kwa wafanyakazi wao wote katika mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na WCFwakiwemo Madereva na kuwasilisha michango yao kwa wakati.
"Kutokana na hayo yote niwasihi viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuzingatia utaratibu uliowekwa kisheria katika kuitisha migomo ya wafanyakazi,".
Na kuongeza Kusema "Nitoe rai kwa Madereva wasio wanachama wa vyama vya wafanyakazi kuacha kutumia njia zisizo halali kisheria kuanzisha ama kuchochea migoma kwani kufanya hivyo ni uvunjaji wa sheria za nchi," alisema
Mwisho







0 Comments