NA CHAUSIKU SAIDM,MATUKIO DAIMAAPP WANZA
wazazi wametakiwa kuwapeleka shule watoto wenye mahitaji maalum ili kupata elimu na kuachana na mila potofu ya kuwafungia ndani na kuwaona watoto hao hawafai kwenye jamii
Rai hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Buhongwa Joseph Bernard wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Asasi ya Tusaidiane wenye lengo la kuelimisha jamii juu ya elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu na kueleza kuwa kila mtu ana wajibu na haki ya kupata elimu.
Bernard ameeleza kuwa serikali inajitahidi kutengeneza miundo mbinu itakayowasidia watoto wenye mahitaji maalum kuweza kujifunza
" Tunajitahidi kujenga majengo ambayo yatawasaidia kupata elimu kwa urahisi na yatakayowawezesha kupita kwa urahisi" Alisema Bernard.
Aidha ameeleza kuwa watoto wenye ulemavu wanauwezo mzuri darasani hivyo hakuna sababu ya kiwaficha ndani na wakakosa haki yao ya maingi.
"Kwa Mungu hakuna mwenye mapungufu kila mtu ni sahihi kwake kwa nini sasa sisi tuwatenge" Alisema Bernad.
Kwa upande wake katibu wa Asasi hiyo ya Tusaidiane Msafiri Msedi ameeleza kuwa elimu jumuishi ni haki kwa wote lakini bado kuna ubaguzi na mitazamo hasi juu ya haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu mbali na serikali kiboresha utekelezaji wa mfumo wa elimu jumuishi.
Msedi ameeleza kuwa watoa maamizi bado hawatimizi wajibu wao wa kisheria pamoja na uwepo wa upungufu wa vifaa vya kujifunzia kama vile karatasi za maandishi ya nukta nundu hali hiyo kupelekea wazazi kushindwa kumudu gharama na mahitaji.
Msedi amefafanua kuwa bado kuna changa moto ya usafiri kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hali inayopelekea kusafirishwa kwenye magari yasiyo salama ambayo hayana miundo mbinu ya kuwawezesha wanafunzi wenye ulemavu.
"Katika mazingira kama haya Wanafunzi wengi wenye ulemavu wako kwenye hatari ya kudhulumiwa haki zao"Alisema Msedi.
Aidha amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mkataba wa kimataifa wa watu wenye ulemavu lakini lakini bado la ukiukaji wa haki za watu wenye ulemavu hususani katika suala la elimu jumuishi.
" hii inakwenda kinyume na kifungu namba 9 cha mkataba wa kimataifa na watu wenye ulemavu kuhusu haki ya kufikia malengo" Alisema Msedi.
0 Comments