Header Ads Widget

WAKANDARASI NA WAHANDISI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

 



NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA


RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Wakandarasi na wahandisi wa miundombinu wa ndani kufanya kazi zao kwa weledi huku wakizingatia ubora na usahihi kwani serikali yake itahakikisha inawatumia katika miradi mbalimbali tena mikubwa inayoendelea hapa nchini.


Rais Samia aliyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa akiongea kwa njia ya simu kwenye kongamano la Wakandarasi na wahandisi wazawa lilioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia kongamano liliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete .


Aliwaomba Wakandarasi kujua kuwa kazi zinazofanyika nchini  ni za maendeleo hivyo lazima kutanguliza uzalendo katika kuzifanya kazi inavyotakiwa.


"Mimi naamini kuwa tukiwapa kazi za ndani ninyi Wakandarasi wa ndani uchumi utakua na mzunguki wa pesa utakuwa Mkubwa pia ,"alisema Rais Samia


Alisema Serikali itakuwa karibu zaidi na Wakandarasi wazawa na tutahakikisha hizi kazi ndogo ndogo na hata miradi mikubwa Wakandarasi wetu mnapata kazi katika miradi hii.


"Kwahiyo ni vizuri kufanyakaazi zenu kwa usahihi kwasababu miradi mikubwa inayokuja ni mingi na  tunataka Wakandarasi wa ndani mshiriki kwa kiasi kikubwa ili kukuza uwezo wenu ,"alisema Rais Samia .


Na kuongeza Kusema" Niwapongeze kwa jambo hili kubwa lakini pia nimeambiwa kuwa mmeniandalia zawadi nawashukuru sana na niwatakie Kila laheli na Serikali ipo pamoja na ninyi," alisema Rais Samia.


Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya alisema barabara zenye urefu wa kilometa zaidi ya 2500 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha rami katika awamu hii ya sita.


Alisema kwa upande wa reli ya kisasa ipo miradi minne inayoendelea ambapo jumla ya kilometa 4752 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Hili ni jambo la kujivunia sana chini ya uongozi wa Rais Samia na tumesikia ushauri mbalimbali wa maeneo ambayo yanatakiwa kuboresha na sisi tumeyachukua tutayafanyia kazi


Alisema Raia Samia kuwa mshindi wa Mwaka 2022 ni matokeo makubwa ya kazi iliyofanywa na Serikali yake na awamu iliyotangulia ni kweli tuzo hiyo inamstahiri  kwa kazi kubwa anayofanya  katika kuboresha,kuimarisha na kujenga miundombinu ya usafirishaji

 

" Hadi sasa Tanzania inamtandao wa barabara za taifa zenye urefu wa kilometa 36,361 ambapo kati ya hizo barabara Kuu ni km 12,215 na barabara za Mikoa ni km 24,146 ," alisema Kasekenya.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI