NA CHAUSIKU SAID ,MATUKIO DAIMA APP
MWANZA.
Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Mwanza wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa ongezeko la mshahara wa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma mkoani hapa.
TUCTA jijini Mwanza wamefanya maandamano hayo leo ambayo yameongozwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamaga Amina Makilagi ambayo yameanzia katika uwanja wa Grand hall na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engineer Robert Gabriel katika ofisi za Mkuu wa Mkoa.
Akisoma risala katibu wa Tucta Mkoa wa Mwanza Zebedayo Athuman amempongeza Rais Samia kwa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa 23.3% ambayo itawakwamua kiuchumi,kibali Cha kuruhusu katika posho kwa watumishi watakaosafiri ndani ya nchi kwa viwango vilivyobainishwa, kuwapandisha vyeo watumishi wa umma 92619 na kuajiri watumishi wapya 12336 ambao wamepunguza uhaba wa watumishi nchini hasa katika sekta ya Elimu na Afya pamoja na kuboresha utumishi wa umma ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia.
"Ombi Kama TUCTA Mkoa wa Mwanza tunaomba jitihada zilizofanyika katika sekta ya umma zifanyike haraka kwa wafanyakazi wa sekta binafsi ambao nao wanastahili kuongezewa mishahara"amesema katibu TUCTA Atuman.
Kwa upande wake mgeni Rasmi mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engineer Robert Gabriel amewataka wafanyakazi wote mkoani hapa kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha wanatimiza malengo kwa serikali na kwa wananchi,kutojihusisha na ubadhirifu wa Mali pamoja na kutojihusisha na rushwa.
"Kila mtu atimize wajibu wake tutakuwa tumempa Rais Samia unafuu"amesema Rc Gabriel.
Ameongeza kuwa watumishi wa umma haki itendeke kwenye ofisi za Tanesco,TRA, Idara ya maji,Halmashauri ya jiji,wahasibu,Manispaa ya Ilemela,waalimu wote hali ambayo itasaidia wananchi kuonesha ushirikiano baina ya ofisi pamoja na wananchi.
Aidha ameongeza kuwa wafanyakazi wote mkoani Mwanza waendelee kumuunga mkono Rais Samia katika kuiletea Taifa la Tanzania maendeleo na kuifungua nchi kiuchumi na kidipromasia.
Nae mmoja wa walimu kutoka jiji la Mwanza Vivian Nyambui amesema kuwa anamshukuru Rais Samia kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata ujauzito,wafanyabiashara wadogo na wakubwa watanufaika pamoja na kumalizia miradi mikakati ya maendeleo.
Sambamba na hayo TUCTA mkoa wa Mwanza wameahidi kwa uadilifu kuchapa kazi muda wote pamoja na kushirikiana na wananchi.
0 Comments