Header Ads Widget

TFF YATAKIWA KUJENGA VIWANJA VYENYE VIWANGO KOTE NCHINI

 

NA RAYMOND MINJA MAFINGA

Wizara ya Sanaa utamaduni na michezo kwa kushirikiana na shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF wameshauriwa kujenga viwanja  vya  Mpira wa miguu vyenye viwango vinavyokubalika kimataifa ili kukuza mchezo wa soka hapa nchini.

Akizungumza na matukio daima mwenyekiti wa Simba wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Methew Mkumbo alisema kwenye mikoa mingi kumekuwa na viwanja vya Mpira wa migu visivyo na uwezo Jambo ambalo litiaa aibu na kushusha hadhi ya soka.


Alisema kuwa TFF ni shirikisho la Mpira wa miguu linaloingiza fedha nyingi kupitia Mpira  hivyo ni vema Wizara kushirikiana na shirikisho Hilo kuhakikisha wanajipanga ili kujenga au kukarabati viwanja ili viwe na viwango na ubora unaokubalika.


"Hii ni aibu kuona tunashindwa kuwa na viwanja vya michezo vyenye viwango Kama hapa mafinga tunao uwanja wa wambi lakini ulee uwanja hauna vigezo vya kuchezesha mashindano Ila huwa tunafanya tu kwakuwa hatuna uwanja mwingine Ila ule uwanjaa haufaii kabisa" 


Mkumbo alisema endapo siku atakuwa hata mjumbe kwenye bodi ya TFF atahakikisha anatumia ushawishi mkubwa kuishawishi bodi hiyo kujenga viwanja vyenye viwango vinavyokubalika kwenye mikoa na hata wilaya.


"Unajua hata sisi wenye viti wa matawi ya Simba na yanga huwa tunakaa na kujaribu kutengeneza vitu vinavyoacha alama Sasa tukiwa na viwanja vizuri tutafanya vizuri,Ila siku nikiwa hata mjumbe kwenye Ile bodi mutaona mabadiliko makubwa kwenye viwanja vyetu vya michezo"


Hata hivyo Mkumbo alisema ubovu huo wa viwanja vya michezo umekuwa ukiwakatisha tamaa vijana chipukizi kukuza vipaji vyao Jambo ambalo linafanya ndoto zao kupotelea hewani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI