Header Ads Widget

MAOFISA MICHEZO NCHINI WATAKIWA KUSAKA VIPAJI VYA MICHEZO KWA VIJANA



RAI imetolewa Kwa maofisa michezo nchini kuepuka kukaa ofisini na badala yake kutoka kwenda kuibua vipaji vya michezo kwa vijana . 

Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa kamati ya nidhamu na mwakilishi wa Mkutano mkuu Taifa toka mkoa wa Pwani ya kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania wakati ule (FAT) sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Karim Mtambo wakati wa kufungua kikao kazi cha maofisa michezo wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kilichoandaliwa na baraza la Michezo Tanzania (BMT).


Naye Msajili wa vyama vya michezo na mashirikisho ya michezo Tanzania kutoka BMT Riziki Majala amesema kuwa kikao hicho ni kwa ajili ya kuwaongezea maarifa na uelewa.


Kwa upande wake ofisa michezo mkoa wa Pwani Grace Bureta amesema kuwa moja ya changamoto ni usajili wa Vilabu, vyama vya michezo na wale wanaoandaa matamasha.


Awali akishukuru kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho ofisa michezo mkoa wa Dar Adorph Halii amesema kuwa watatumia mafunzo hayo kuibua vipaji.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI