Header Ads Widget

KAMANDA MUTAFUNGWA AONYA MADEREVA MWANZA

 


Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani  Tanzania (SACP )Wilbroad W. Mutafungwa   amezungumza na Madereva na abiria stendi ya mabasi  Buzurugwa wilaya ya  Ilemela  mkoani Mwanza kuwataka wazingatie sheria za usalama barabarani.

Mutafungwa ambae aliambatana na SO (M) Mwanza ACP G.K MSUYA Kaimu Rto Mkoa wa Mwanza  ASP F.J. MPOLO pamoja na Wakuu wa Polisi Usalama Barabarani wa Wilaya(DTOs) za Misungwi, Ilemela, Sengerema, Magu  aliwataka madereva hao Kutii wa sheria bila shuruti.

Kwa kuhakikisha Kila dereva anazingatia sheria za usalama barabarani kwa kutotembea kwa mwendokasi na wrong kuovateki , ambapo pia aliwaeleza kuwa amewaelekeza askari kusimamia kikamilifu sheria kwa kutokuwa na muhali na madereva wenyekufanya makosa ya namna hiyo, na kwa wale madereva sugu wafanyao makosa ya kujirudia rudia wachukuliwe hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwaweka mahabusu na kutokea mahabusu kuwapeleka mahakani



Pia aliwataka abiria kutokuwatetea madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kupiga namba za simu zilizobandikwa kwenye mabasi hayo ili waweze kuchukuliwa hatua na wao kuweza kusafiri salama.


Pia Mutafungwa  alibandika namba za kutolea taarifa kwa abiria kwenye mabasi matatu na kuyaruhusu kuendelea na safari. Habari picha kuhusiana na tukio hilo zahusika hapa chini;


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI