NA RAYMOND MINJA MATUKIO DAIMAAPP MAFINGA
Jumla ya watu 19 wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajari iliyohusisha Lori aina ya scania na coster iliyotoka eneo la changarawe wilaya ya Mufindi mkoani Iringa alfajili ya leo.
Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Scania yenye namba za Usajiri T 736 AAE na Coaster yenye namba za usajiri T542 DQV
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mafinga Dr. Victor Msafiri alisema kuwa ajali hiyo iliyotokea imesababisha vifo vya watu 19 na majeruhi ambao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospital hiyo.
Alisema kuwa Majeruhi wanaendelea kupata matibabu na miilii ya marehemu baadhi imeshatambulika na wengine wanaendelea kutambuliwa na jeshinla polisi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafinga mjii Bi, Happiness Laizer amewatembelea majeruhi na kuwapa pole huku akiwaomba madaktari kuwapa hudumu stahiki ili Hali zao ziweze kutengemaaa
0 Comments