Header Ads Widget

TIRA YAZIPIGA FAINI KAMPUNI NNE ZA BIMA

 


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam


Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Tanzania (TIRA) imezipiga faini kampuni nne za bima kwa kukiuka sheria za bima namba 10 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake.


Akizitaja kampuni hizo ni pamoja na kampuni UAP, Jublee Insurance, Insurance Group of Tanzania IGT huku kampuni ya Resolution Insurance ikiwekewa zuio la kutoendelea kuandikisha, kufanya matangazo na kuchukua biashara yoyote mpya kuanzia sasa.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamshina wa TIRA Dr Baghayo. A.Saqware amesema Soko la bima la Tanzania licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo lakini linaendelea kukua kwa asilimia 10, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kwani mamlaka hiyo inafanya kazi zake kwa kufiata sheria.


Akizitaja kampuni hizo ni pamoja na kampuni ya bima ya Insurance Group of Tanzania (IGT) ambayo imepigwa faini ya shiling mill 20 ambapo Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu, Afisa fedha Mkuu pamoja na Meneja wa madai na fidia wakitakiwa kulipa kila mmoja shill mill 5.


Amesema kuwa, hatua hiyo imekuja kwa kuzingatia kifungu namba 166(1) cha sheria ya bima nchini ambayo pia imeiagiza kampuni hiyo kulipa wadai wote 48 ambao imeshawapatia hati ya kukubali madai ndani ya siku 14.


Pia ameipiga faini kampuni ya Jublee shi mill 5 ambayo tayari  imeshalipwa huku ikiamuru kampuni hiyo kulipa fidia ya kiasi Cha Uro mill 511 kama inavyodaiwa na Wizara ya maji baada ya kampuni ya ukandarasi ya Spencon kushindwa kutimiza wajibu wake wa kimkataba wa miradi ya maji wenye mkataba namba ME-011/2011-2012/W/O5 kwa Mamlaka ya maji ya mji wa kigoma ambao ulikua umepewa Kinga na kampuni ya Jublee.


Hata hivyo, pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jublee amepigwa faini ya shill mill 10 kwa kutofuata taratibu za kibima hivyo, kupelekea kuchafua taswira ya Soko la bima nchini.


Aidha mamlaka ya bima inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kampuni zote za bima nchini zitatakiwa kuleta taarifa za madai yote yaliyowasilishwa kwa watu za kiutendaji au usuluhisho walizofikia kila robo ya mwaka .


Pia TIRA wamewaasa watanzania kuendelea kutumia huduma za bima nchini na kutosita kuleta malalamiko yao kwa kamishna wa bima pindi wanapoona kampuni za bima haziwatendei haki.


Kutokana na Mamlaka kuwa na jukumu la kulinda watumiaji wa bima inatoa onyo kwa kampuni za bima nchini zitakazochelewesha ama kuchezea haki ya fidia ya mwananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI