Teddy Kilanga_Arusha
Kutokana na ugonjwa wa aina ya Brucella kuenea na kuathiri zaidi binadamu na wanyama,Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela(NM-AIST) imeanza mpango wa kudhibiti ugonjwa wa Brucella kwenye Halmashauri ya Meru iliyopo Mkoani Arusha na Hai Mkoa wa Kilimanjaro
Akizungumza katika warsha ya wadau wa Ng'ombe wa maziwa kutoka halmashauri hizo,Mratibu wa Mradi wa Mpango wa Kupima na Kuhakiki Ugonjwa wa Brucella katika Halmashauri za Meru na Hai,Profesa Gabriel Shirima alisema mradi umeanza katika Halmashauri mbili kwenye Mkoa wa Kanda ya Kaskazini kwasababu ndio wazalishaji wakubwa wa maziwa na kwa Tanzania ndio wa kwanza.
Aidha alisema kwamujibu wa tafiti za kitaalam zilizofanywa na watafiti wameamua kuja na mpango huo wa kupima sampuli za maziwa kwa wafugaji wa wilaya hizo mbili kisha kupewa vyeti vya muda ili badae maziwa hayo yaweze kununuliwa kwa wafugaji kupitia mashamba darasa.
"Nitoe rai kwa wafugaji watakaoanza mradi huu ndani ya wilaya hizi kuhakikisha wanaanzisha mashamba darasa ili kulisha mifugo yao kisha Taasisi ya Nelson Mandela itatumia maabara zake kwaaajili ya kupima sampuli za maziwa hayo kama yapo salama au la,"alisema Profesa Shirima.
Pia aliongeza kuwa kwa upande wa wafugaji watakaoingia katika programu hiyo katika halmashuri hizo watapewa vyeti vya utambulisho vya muda na ikidhibitika maziwa yao ni Bora kupitia mashamba darasa yaliyoanzishwa baada ya kupima katika maabara watapewa vyeti vya uhakikisha maziwa yao kununuliwa na wananchi ili waweze kuyatumia kama lishe au kinywaji chenye usalama.
Vilevile alisema ugonjwa wa brucella unaleta athari kwa wafugaji na watumiaji ambapo utoka kwa wanyama aina ya ng'ombe na huanaambukiza binadamu hivyo wameanza kudhibiti ugonjwa huo kwa kuanzia halmashauri hizo mbili na baadaye utaendelea kwingine.
Hata hivyo alisema wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ambayo ni lishe na ulishaji ikiwemo maradhi ya mifugo ,mifumo ya masoko na mazao ya mifugo hiyo
Awali alieleza programu hiyo ni wazo walilokuwa nalo muda mrefu ndani ya Wizara ya mifugo na Uvuvi wakaona waanzie katika wilaya hizo mbili ikiwa Mkoa wa Njombe ukiwa umeonyesha nia hizowasababu ya ugonjwa huo unaathiri zaidi binadamu.
Alieleza utekelezaji wake Mratibu huyo alisema baada ya vijiji kuanishwa watachukua sampuli na kutoa vyeti vya muda wa miaka mitatu na shamba litakalothibitika kutokuwa na tatizo hilo maabara ya Nelson is itapima sampuli za maziwa na kisha matokeo kutolewa kupitia maofisa mifugo husika ili kupewa matokeo chanya na ukienda vema utasambaa maeneo mengine kwaaajili ya kuleta tija kwa wafugaji.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Cha Taaluma,Utafiti na Ubunifu, Profesa Anthony Mshandete alisema tasnia ya maziwa ni uwanda mkubwa hivyo Wizara ya Mifugo na Uvivu imeona sekta hiyo ni muhimu lakini inakabilna changamoto mbalimbali
Alisema upimaji huo wa brucella kwa ng'ombe wa maziwa utasaidia kudhibiti maambuikizi ya binadamu na mifugo hivyo wizara inachukua hatua mbalimbali za kimkakati kudhibiti
Profesa Mshandete aliipongeza Taasisi ya Nelson Mandela kupima kwa kuanzidha mradi huo utakaowasaidia wafugaji kuepukana na ugonjwa huo kutokana na kupata uvumbuzi utakaosaidia katika kudhibiti.
Wakati huo huo,baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Samwel John kutoka Hai walishukuru programu hiyo kuanzishwa ili kudhibiti Ugonjwa huo unaoleta athari kwa binadamu na mifugo
0 Comments