Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kuzungumza na Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji mjini Pemba, Msumbiji.
Dkt Kikwete nchini Msumbji kwa shughuli za Allience for a Green Revolution in Africa (AGRA), shirika linalojihusisha na mageuzi ya kilimo cha wakulima wadogo Barani Africa ambalo yeye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
Vile vile Rais Mstaafu Dkt Kikwete yupo huko Msumbiji kwa shughuli za jopo la wazee wa SADC (SADC Panel of Elders) linalojishughulisha na kusuluhisha migogoro na kuleta amani kwa nchi wanachama wa SADC ambapo yeye ni Mwenyekiti wake.
0 Comments