Header Ads Widget

NMB YAJA NA MKAKATI MPYA WA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI WADOGO



Na Teddy Kilanga ,Matukio Daima APP Arusha 

Taasisi ya kifedha(NMB) yazindua kampeni ya aina ya Teleza kidigitali katika kanda ya kaskazini wenye lengo la kusogeza huduma kwa wananchi ili waweze kumia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo nafuu.


Akizundua mfumo huo,Afisa mkuu wa biashara na wateja binafsi wa NMB Filbert Mponzi alisema mfumo huo wa Teleza kidijitali  ni kampeni ambayo inasaidia kuwasogeza watanzania wengi kuingia katika mfumo wa kibenki hali ambayo itaokoa muda kwa wateja katika kufuata huduma katika matawi ya NMB.



Aidha alisema kupitia mfumo huo wananchi hawatakuwa na ulazima kufika kwenye matawi ya NMB kufanya miamala lakini kupitia mshiko fasta ambao ni mkopo wa wateja wadogo wadogo na inayopatikana kwa njia ya NMB mkononi.



"Hii ni mteja atafungua akaunti na kutokana na miamala yake anaweza kujipatia mkopo wenye takribani sh.laki tano lakini pamoja na hilo tunamletea mawakala wetu wa NMB pesa,"alisema.



Alisema lakini wale wenye sehemu zao za biashara NMB inatoa huduma ya lipa mkoni ambapo inamwezesha mfanyabiashara mjasiriamali kuweza  kulipwa pesa zake za mauzo na hiyo itamrahisishia pesa zakr kwenda moja kwa moja kwenye akaunti.



"Lengo kubwa zaidi tunataka wananchi wengi kuingia katika mfumo wa kibenki na kutokana benki ya NMB ni benki iliyotapakaa kila mahali itakuwa na mchango mkubwa sana katika kuhakikisha inawahudumia wananchi wengi zaidi,"alisema Mponzi.



Nao baadhi ya wafanyabiashara hao wa soko la Kilombero walisema wanaishukuru benki ya NMB kwa kuwaletea hudumu hiyo itakayowasaidia kupata mikopo ya fedha kwa ajili ya kujiinua kichumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI