Header Ads Widget

MILIONI 121 ZAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI PAROKIA YA UTALINGOLO

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima APP,NJOMBE

Kiasi Cha zaidi ya shilingi Milioni 121 kimefanikisha ununuzi was Gari jipya aina ya Land cruser Hard top kwa ajili ya utoaji huduma za kichungaji Katika parokia ya Utalingolo Jimbo Katholiki la Njombe kutokana na kuwapo kwa Changamoto ya uhaba wa Vyombo vya usafiri.

Taarifa ya Makabidhiano ya Gari Hilo Katika kanisa Hilo  iliyosomwa na Katibu mkuu wa kamati hiyo bwana Deogratias Mtewele imesema fedha hizo zimetokana na michango Mbalimbali ya waumini,Wadau wa maendeleo Pamoja na wafadhali toka Nje ya Nchi.

Mwenyekiti wa kamati ya Uhamasishaji wa ununuzi wa gari Hilo Bwana Erasto Mpete ambaye Ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe na diwani wa kata ya Utalingolo anasema haikuwa kazi rahisi kupatikana kwa chombo hicho Cha usafiri Huku akitoa wito kwa Uongozi wa kanisa.


Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deodatus Mwanyika katibu wa Mbunge huyo Andreas Mahali anasema ushirikiano wa Pamoja ndio unaowafikisha mbali Wananchi kimaendeleo Kama walivyoshirikiana kununua Gari Hilo.

Mwanasheria wa mkoa wa Njombe Hilmar Danda akimwakilisha mkuu wa mkoa anasema Ni lazima serikali iendelee kuziunga mkono dini zote licha ya kuwa Yenyewe Haina Dini.

Padre Athanas Mgimba kwa niaba ya  Askofu Jimbo  Katholiki la Njombe anasema kila muumini wa kanisa Katholiki Utalingolo anapaswa kuwa mlinzi wa Gari Hilo Huku paroko wa parokia hiyo Padre Lukas Mgaya ameshukuru jitihada zilizofanyika Hadi kupatikana kwa Gari Hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI