Header Ads Widget

MCHONGOO KUIBUA FURSA

 

Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam

Katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini Tanzania, Kampuni ya mchongoo.com imeanzisha jukwaa maalum la kutoa huduma zaidi ya 155 ambazo zinakwenda kutoa fursa kwa watanzania mbalimbali.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar er Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Julius Wambogo amesema kuwa mitaani watu wengi wamesoma fani mbalimbali na wengine wanaujuzi wa kufanya shughuli mbalimbali lakini hawana ajira yoyote hivyo, kuanzisha kwa jukwaa hilo kutakwenda kusaidia watu wengi wenye uhitaji.


Amesema kuwa, kujiunga na website ya Mchongoo ni bure lengo ikiwa ni kuwezesha watu wengi kuweza kupata fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika jukwaa hilo, huku miongoni mwa sharti la mtu kuomba kutuo huduma zake ndani ya jukwaa hilo ni lazima atoe kitambulisho chenye picha yake na majina kamili.


"Kujiunga ni bure lakini lazima mtu aweze kutuma kitambulisho chake ambacho kitakua na majina yake kamili na picha yake, pia tutaweza kumfanyia mahojiano ya dakika tano atakapo kidhi vigezo tutaweza kumsajili hii yote ni kuhakikisha usalama wa huduma tutakazozitoa ndani ya jukwaa letu"amesema Wambogo.


Aidha, amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga na Mchongoo Appy, huku akizitaka kampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi kutumia jukwaa hilo kujipatia wataalamu mbalimbali, wakiwemo watu wa IT. 


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa GetCore Group LTD, Fayaz Damond Valli amesema kuwa Mtandao huo mpaka sasa umeweza kuhudumia zaidi ya watu 300 ndani ya miezi mitano  tangu kuanzishwa kwake ambapo huduma mbalimbali zinatolewa , hivyo watu waweze kujisajili ili kutoa huduma zao.


Aidha amesema lengo la kampuni hiyo ni kuweza kuzunguka mikoa yote nchini Tanzania ambapo kwa sasa wameanzia kwa Mkoa wa Dar es Salaam huku nafasi 155 ya huduma ya huduma mbalimbali zikihitajika kutolewa katika jukwaa hilo ikiwa ni pamoja na Mpishi, waosha magari, wapiga picha pamoja na waigizaji.


Aidha, amesema licha ya kufanya kazi nchi ya Tanzania lakini wanataraji kukuza mtandao huo katika ukanda wa East Afrika pamoja SADC kutokana na watu wa mataifa hayo kuwa na muelekeo sawa katika harakati za kimaisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI