Header Ads Widget

HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA RUVUMA YAPOKEA VIFAA TIBA VYA TEKNOLOJIA YA KISASA


 Na Amon Mtega,Matukio DaimaAPP Ruvuma 

HOSPITALI ya Rufaa ya mkoa Songea   imepokea vifaa tiba vya teknolojia ya kisasa vitakavyotumika kwa njia ya mtandao kutambua tatizo la mgonjwa kabla hajapatiwa rufaa ya kwenda Hospitali za ngazi ya juu zaidi ili kupunguza adhaa zilikuwa zikiwakabili wagonjwa hao.


 Akipokea vifaa hivyo toka Wizara ya Afya Mganga mkuu mfawidhi wa Hospitali ya rufaa  Songea Dk.Magafu Majura amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kupunguza changamoto za baadhi ya wagonjwa ambao walitakiwa wakatibiwe Hospitali za ngazi ya juu kwa gharama kubwa.


Dk Majula amefafanua kuwa vifaa hivyo vitafanya kazi kwa njia ya mtandao kupiga picha ya ugonjwa kwa mgonjwa kisha kutuma kwa madaktari bingwa katika Hospitali mbalimbali ikiwemo Muhimbili na madaktari hao hutoa majibu nini cha kumtibu mgonjwa bila kumsafirisha kumpeleka kwenye Hospitali hizo.


Amesema kuwa katika kipindi cha nyuma kabla ya huduma hiyo ya matibabu kwa njia ya mtandao kulikuwa na kazi ya mgonjwa ambaye amepatiwa rufaa ya kwenda Hospitali kubwa kama Muhimbili kusafirishwa kwa umbali mrefu jambo ambalo lilikuwa ni kero kwa wagonjwa.


Majula amesema kuwa wagonjwa ambao watapelekwa kwenye Hospitali za ngazi ya juu zaidi ni wale ambao watakao ruhusiwa na madaktari bingwa wa Hospitalini hizo kuwa waende wakaangaliwe tatizo lao kwa karibu zaidi.


Kwa upande wake Dkt Liggie Vumilia mratibu wa tiba mtandao katika Wizara ya Afya amesema kuwa Wizara kwa kuanzia imepeleka vifaa hivyo katika Hospitali za rufaa tano ikiwemo ya Songea Mkoani Ruvuma na kuwa utaisaidia kupunguza gharama zilizokuwa zikiwapata wagonjwa kwa kusafiri umbali mrefu kuzifuata Hospitali za ngazi ya juu.


Dkt , Vumilia amesema kuwa wataalamu wakutumia vifaa hivyo tayari wameandaliwa kikamilifu na kuwa itasaidia kupunguza msongamano uliyokuwa ukitokea kwenye Hospitali hizo ambazo huchukua wagonjwa wa kutoka maeneo mbalimbali ya Nchi.


Naye kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Wizara ya Afya Catherine Sungura amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaenda kupunguza changamoto za kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya ambapo sasa mabadiliko makubwa yanatokea.

     Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI