Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa wa Njombe Kimetoa Tahadhari Kwa Wakulima Kutouza Mazao Yote Pindi Watakapovuna Kutokana na Kuwapo Kwa Mabadiliko Makubwa ya Tabia Nchi Yaliyosababisha Mvua Kuwa Chini ya Wastani.
Mbele ya Vyombo Vya Habari Kaimu Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Njombe Stanley Mbembati Anasema Kama Chama Kinayo Nafasi ya Kuwashauri Wakulima Ili Wasikumbane na Baa la Njaa Hapo Baadaye.
Sanjari na Kuwashauri Wananchi na Wakulima Kuchukua Tahadhari Juu ya Hali ya Hewa Kama Ambavyo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Ilivyotabiri Lakini Mwenyekiti wa Chama Hicho Mkoa Ally Mhagama Anasemea Kama Chama Cha Siasa Kitaendelea Kushirikiana na Jamii Wakati Wote Kwani Kingali Kipo Imara Hata Kuelekea Katika Uchaguzi Mdogo wa Diwani wa Kata ya Njombe Mjini.
Kituo Hiki Kimezungumza na Baadhi ya Wakulima na Wanunuzi wa Mahindi akiwemo Chesco Ng'wabi,Nickson Mgeni na Mzee Cosmas Msigwa Toka Magoda Wanakiri Kuwapo Kwa Uhaba wa Mvua Ambao Umesababisha Baadhi ya Mahindi Kukauka Kwenye Baadhi ya Maeneo.
Sady Mwang'onda ni Mtaalamu wa Kilimo Toka Kampuni ya Mtewele General Traders Ambaye anaweka Wazi Sababu za Mabadiliko ya Tabia Nchi na Hatua Zinazopaswa Kuchukuliwa na Wakulima.
0 Comments