Header Ads Widget

ZAIDI YA SH.MILIONI 703 ZIMETUMIKA HALMASHAURI MBINGA MJI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI 6 YA MWENGE.

 



NA AMON MTEGA, _MBINGA.


ZAIDI ya Shilingi Milioni 703 zimetumika katika utekelezaji wa miradi sita ikiwemo ya sekta binafsi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mbinga mji Mkoani Ruvuma.


 Akitoa taarifa ya miradi hiyo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma ,mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo ameitaja miradi hiyo pamoja na garama zake .


 Mangosongo ameitaja miradi hiyo kuwa ni wa  kufungua na kuzindua kiwanda cha kusindika unga wa Sembe ambacho cha mtu binafsi (AMNEC),mradi wa kituo cha Afya cha Mtakatifu Gabriel kinachomilikiwa na misheni ya Mbinga kuweka jiwe la msingi huku mradi mwingine kuwa wa kufungua na kuzindua ujenzi wa madarasa ya TCRP 5441 katika shule ya Sekondari ya Luhuwiko.


Akiendelea kutaja miradi mingine kuwa ni kufungua na kuzindua mradi wa Anuani ya makazi na post kodi uliyopo kata ya Mbinga 'A' kuzindua na kufungua mradi wa klabu ya wapinga Rushwa iliyopo chuo cha maendeleo ya Wananchi (FDC)kutembela mradi wa kikundi cha Ujikwamue cha Vijana waendesha pikipiki (Bodaboda) ambao mradi huo ulishauriwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma kuwa ukamilishe kwanza taratibu zote za vyombo vya Moto.

 


 Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma baada ya kupita kwenye miradi hiyo ameitaka Halmashauri ya Mbinga mji kushughulikia kikundi cha Vijana waendesha pikipiki kwa kufuata taratibu zote huku akifurahishwa na miradi mitano ya awali kuwa ni miradi yenye tija.

     

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI