Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma.
KUTOKANA na Muingiliano mkubwa wa nchi ya Tanzania na nchi jirani ya Malawi imebainika kuwa kunauwezekano mkubwa wa kufika kwa ugonjwa wa Polio ambapo watoto wote wenye umri wa miaka 0 hadi 5 wanatakiwa kufika katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili kuweza kupatiwe chanjo hata kama walishapata hapo awali.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 13,2022 jijini hapa na Mganga Mkuu wa Mkoa Best Magoma katika kikao cha afya ya msingi cha Mkoa kilichowakutanisha wataalam pamoja na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali katika jamii .
Mganga Mkuu wa Mkoa Magoma, amesema chanjo hizo tayari zimesambazwa kwenye kila halmashauri na hiyo ni kutokana na tishio la uwepo wa ugonjwa huo katika nchi jirani.
" Niitake jamii kujitokeza kwa wingi kwa kuwapeleka watoto wenye umri kati ya mwaka 0 hadi 5 kupata chanjo ya ugonjwa wa polio ambayo inatarajia kuanza rasmi Aprili 28 mpaka Mei 1,2022 ikiwa ni kampeni maalum ya kitaifa ya chanjo ya ugonjwa wa Polio,"amesema Dkt Magama
Hata hivyo, amesema maandalizi mbalimbali ya uhamasishaji ya kuwapa wananchi uelewa tayari yameanza lengo likiwa ni kuwafanya wananchi wajitokeze kwa wingi kuwapeleka watoto na kuachanacha na dhana potofu ya kuogopa chanjo .
Kwa upande wake Ofisa wa ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko Dkt. Haika Kimambo kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) amesema serikali imeamua kufanya kampeni hiyo kutokana na ugonjwa wa polio kutokea katika nchi ya Malawi Novemba mwaka jana 2021.
“Kutokana na usambaaji wa ugonjwa huu kwa haraka awamu ya kwanza chanjo hii ilifanyika katika mikoa ya Njombe,Iringa, Ruvuma ,Mbeya pamoja na Songwe na hii inayotarajia kuanza Aprili 28 itahusisha nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Visiwani," amesema Dkt, Kimambo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabiri Shekimweri,amesema kama Mkoa tayari umepokea chanjo laki 551,000 za ugonjwa wa polio na matarajio ni kuchanja watoto laki 4 79,000 ambapo kwa Dodoma jiji matarajio ni kuchanja watoto elfu ,77,000 na chanjo elfu 88,000 tayari zimepokelewa.
“Uchanjaji huu ni salama na sio mara ya kwanza wananchi kuchanja chanjo ya ugonjwa huu hivyo wananchi jitolezeni kwa wingi kushiriki kwenye kampeni hii ya kitaifa kikamilifu lakini pia nitumie fursa hii pia kuwaasa wazazi wawazingatie watoto pale wanapo jisaidia haja wahajikishe watoto wanajisaidie sehemu ambazo si rasmi”amesema Shekimweri.
KwaUpande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda amesema chanjo ya polio ni chanjo muhimu kwasababu wapo baadhi ya watoto ambao hawajapata chanjom hioyo wakiwa wadogo na matokeo yake wamesababishiwa ulemavu wa kudumu hivyo kila mzazi kwa sasa anao wajibu wakumpeleka mtoto kupata chanjo hiyo.
“Tunawashukuru sana wadhamini wetu JAPAIGO kwa kushirikiana nasi katika kampeni hii ya ugonjwa wa Polio na kama Wilaya ya Bahi sisi tayari tumeshapokea chanjo elfu 50” amesema Munkunda
Hata hivyo kikao hiko kimeweza kuwakutanisha viongozi katika ngazi ya mkoa, wajumbe kutoka ngazi ya Wilaya wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri na Makatibu Tawala na Wakurugenzi Lengo likiwa ni kuwashirikisha kampeni hiyo ya uchanjaji ya chanjo ya kujijinga na ugonjwa wa Polio kwa watoto
0 Comments