Header Ads Widget

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI WAPEWA MAELEKEZO HAYA NA WAZIRI MKUU

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwathamini Maafisa Utamaduni Sanaa na Michezo  na Idara nzima kwa ujumla huku akimtaka Katibu Mkuu Dkt Hassan Abbasi kulifikisha suala hilo wizarani haraka iwezekanavyo.


Akiongea leo April 5 ,2022 jijini hapa katika kikao cha 13 kikao kazi Cha Maafisa utamaduni na michezo Tanzania bara waziri Majaliwa amesema Halmashauri zetu zimekuwa zikiwapangia kazi ya kilimo Maafisa Michezo na Utamaduni wakati sio kazi zao na  wengine  wakidiliki kuwapa kazi zingine za Halmashauri hata kama sio za uparesheni na kuwaachisha kazi zao za utamaduni na Sanaa.


Pia amesema hata Mabaaraza ya madiwani yamekuwa hayajadili masuala ya utamaduni Sanaa na Michezo kwenye vikao vyao vya mabaraza ya madiwani na badala yake wamekuwa wakijadili masula mwengine na kusahau kuwa Michezo Sanaa na Utamaduni  zinamchango Mkubwa wa maendeleo ya Taifa letu katika kila Sekta 


Aidha amesema,Utamaduni Sanaa na Michezo ni Afya na inajenga mshikamano miongoni mwa jamii kwani huwezi kupata maendeleo ya Watu waliopagalanyika na Maafisa utamaduni Sanaa na Michezo ndio wamekuwa wakiweka jamii ikae Pamoja.


" Niwatake Tamisemi hakikisheni mnatambua kitengo hiki kuwa ni moja Kati ya kitengo muhimu ndani ya Halmashauri pia wapeni nafasi Maafisa utamaduni Sanaa na Michezo ya kutumia taaluma yao na Majukumu ya katika kutekeleza ndani ya Halmashauri Ili tuone mafanikio," amesema waziri Majaliwa.


Awali akiongea katika kikao kazi  hicho cha nchi nzima Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema sekta hiyo imekuwa ikichangia katika kukuza utalii kwa kuitangaza vyema nchi ya Tanzania na kulipatia Taifa fedha za kigaeni bila kusahau Utunzaji na ufadhi wa Mazingira wa nchini


Hata hivyo amesema ukuaji wa sekta hiyo inatokana usimikizi thabiti na imara na Mazingira wezeshi yanaayotengenezwa kutoka kwa Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan hivyo wadau waseta hizo kuweza kufanya kazi zao zenye tija na Kusimimiwa na Maafisa utamaduni na Michezo ambayo kulingana na kesera ya utamaduni sera ya mwaka 1997 inawaelekeza kusimimia shughuli za kitamaduni ulithi,Mila, destuki historia, lugha na Sanaa katika mikioa na Maalaka ya Serikali za mitaa ambapo ndipo kwenye wadau wengi walipo.

" Kikao kazi hiki ni cha nchi mzima kwani wawakilishi wa kila Mkoa Wapo hivyo tunaimani ujumbe mafunzo na maelekezo yatakayotolewa katika kikao hiki  kitawafikia wadau wote nchini ,"amesema .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI