Header Ads Widget

WAKAGUZI WA NDANI WAFUNDWA

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


NAIBU Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Injinia Andrea Kundo amesema kazi Kubwa ya wakaguzi wa ndani ni kutoa hakikisho juu ya ufanisi wa mifumo ya udhibiti menejimeti ya vihatarishi na mifumo ya utawala hasa katika usimimizi wa matumizi ya fedha ya Serikali na kutathimini utekekezaji wa malengo ya Taasisi.


Akiongea na wakaguzi wa ndani Leo jijini hapa amesema wizara imeandaa kikao kazi hicho lengo likiwa ni kupata uelewa wa Pamoja na kuandaa Mpango kazi wa ukaguzi wa uparesheni wa anuani za makazi utakao saidia na kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa.


"Niukweli kabisa tunafahamu wakaguzi wa ndani mko vizuri elimu zenu zinaoonyesha mko vizuri uzoefu wenu hatuna Shaka nao ijapokuwa tunajali kushea uzoefu katika zoezi hilo kwa sababu sisi wizara tumeanza nalo mwaka 2010 na Tunajua wapi tunaweza na mianya na wapi kuna changamoto tunayokutana nao  hapa wakianza kurukaruka tutawabaini ," amesema  


 "Hayo ni matakwa ya Ilani ya chama cha mapinduzi katika kurasa wa 98 ibara Ya 61 (M) inasema serikali ya chama cha mapinduzi itahakikisha inaweka anwani za makazi Ili kurahisisha utoaji na ufikishaji wa huduma kwa Wananchi Lakini pia ni matakwa ya sera ya Shirika la posta ya Mwaka 2003 na ni makubaliano ya kikanda na kimataifa," amesema .


Aidha amesema  zoezi hilo linatarajiwa kutekeleza kwa Kipindi Cha miaka mitano Rais Samia Suluhu Hassan amesema zoezi hilo linawenda kufanikiwa kwa muda wa miezi 5 


"Leo tuko hapa kwa sababu ya kujengeana uelewa jambo ambalo lilitakiwa kufanyika kwa muda wa miaka 5 tunatekeleza kwa miezi 5 maana yake tunahitaji ufanisi kwa sababu tunatambua mambo hayatakwenda sawa palipo na uharaka wa jambo mambo mengi vya hovyo yanaoneka kutokea.


Amesema anafahamu kazi Kubwa inayofanywa na wakaguzi hao katika mikoa na wizara lakini zoezi hilo limekuja upekee hivyo wanatakiwa wajipange utaratibu waliokuwa wanatumia wataenda. Kuubadili Ili kuendana na kasi ya Mradi unavyotakiwa kutekelezwa.


" Tukiweza kufanya hivyo Basi tutafanikiwa na fedha ambazo amezishusha na Rais wetu Samia za jumla ya Shilingi Bilioni 27.3 kwa Upande wa Tanzania bara na Shilingi Milioni 622 kwa Upande wa Tanzania Zanzibari tukahakikishe tunazitumia kwa weledi Mkubwa  Sana kwasababu sina Shaka na weledi wenu isiyokuwa nawaomba mkaongeze juhudi za kusimamia na kuratibu vizuri jinsi Mfumo utakavyo takiwa kufanyika,"amesema


Amesema utekekezaji wa Mfumo huo wa anuani za makazi ulianza Mwaka 2010 na ulikuwa ukitekelezwa kila Mwaka na ulikuwa ukisuasua hadi pale Rais ulipobadilishwa na kuwa Mfumo wa Uparesheni 


Joyce Christopher mkaguzi wa ndani Mkuu wa wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema lengo la kikao hicho Ni kupata uelewa .


Hata hivyo amesema wameandaa kikao Cha wakaguzi wa ndani wa mikoa yote 31 lengo la kikaoo hicho watapitishwa katika miongozo mbalimbali inayotuka katika uparesheni ya anuani za makazi.


"Rais Samia alielekeza zoezi hilo likamilike ifikapo mwezi May Ili kuweza kusadia zoezi la Sensa ya Watu na makazi kila mwananchi awe na anuani za makazi hivyo sisi kama wakaguzi wa ndani tunajukumu la kuwashauri Maafisa Masuhuli kuhusu utoshelevi na ufanisi wa mifumo ya  ndani menejimeti ya mifumo hatarishi na mifumo ya utawala," amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI