NA HADIJA OMARY MATUKIO DAIMA APP,LINDI
ZAIDI ya asilimia 90 ya akinamama wajawazito Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wanadaiwa kutumia Dawa za Asili kwa ajili ya kuongeza njia za uzazi na kuongeza kasi ya uchungu jambo ambalo ni hatari kwa Afya zao na Watoto walio tumboni
Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ruangwa Mjini Dkt, Ezekia Ambikile alipokuwa anazungumza na Matukio Daima ofisini kwake ilipotaka kujua namna gani matumizi ya Dawa hizo yanavyo hatarisha Maisha ya mama na mtoto alie tumboni
DKT. Ambikile alisema kuwa tatizo hilo la matumizi ya Dawa za Asili kwa akina Mama wanaokwenda kujifungua katika maeneo mbali mbali ya vituo vya afya na Zahanati kwenye Halmashauri hiyo ni kubwa, kwani kati ya akina Mama 10 wanaokwenda kujifungua 6 utumia dawa hizo ambapo wamama 3 kati yao ulazimika kufanyiwa upasuaji kutokana na hali ya uchungu wanaofika nao
Alisema Dawa hizo kwa akina Mama hao zimeonekana kuwa na ufanisi mkubwa kwao kwani wanapofika kwenye Vituo hivyo vya kutolea Huduma wanakuwa na uchungu mkali ambo wakati mwingine uhatarisha Maisha ya mama na Mtoto alie tumboni
“ kibaya zaidi kuna akina Mama wengine ambao wanatumia Dawa hizi wakiwa hawana vigezo vya kutumia kiasi kwamba njia inakuwa haitoshi lakini wanakuwa washatumia Dawa hizo kwa matumaini kwamba atazaa kwa njia ya kawaida ambapo wengine wanakuwa wameshafanyiwa oparesheni za Awali , jambo ambalo kwa Mama ambae alishafanyiwa oparesheni atakiwi kutumia Dawa yoyote ya uchungu huku njia ambayo ni muafaka kabisa inayoweza kumsaidia kujifungua ni kufanywa oparesheni nyingine”
DKT. Ambikile alieleza kuwa jambo lingine la hatali ni kwamba akina Mama waliowengi ufika hospitarini mfuko wa Uzazi ukiwa katika hatua za Mwisho za kuchanika na wengine ufika wakati mfuko huo umeshachanika tayari hali inayopelekea Mtoto alie tumboni kupoteza Maisha.
Sheby Likalame Mkazi wa mtaa wa Nachingwea Halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi alisema kuwa dawa hizo ni za Asili za urithi kutoka kwa Mababu zao na kwamba wamekuwa wakizitumia vizazi na vizazi pindi tu wanapokuwa wajawazito.
Alisema kwa kutumia Dawa hizo wamekuwa wakipata urahisi wakati wa kujifungua kwamba uchukua muda mfupi toka uchungu unapoanza mpaka mtoto kuzaliwa
Nae Mwanahamisi Ahmadi Muuguzi wa Mama aliekuja kujifungua katika kituo hiko cha Afya Ruangwa Mjini aliieleza Matukio daima kuwa wamekuwa wakitumia dawa hizo pindi wanapokuwa na ujauzito kuanzia miezi saba , nane mpaka miezi tisa Mama anapokenda kujifungua huku matumizi ya Dawa hizo yakitofautiana baina ya mtu na mtu
“Dawa hizi tunazitumia Mimba inapofikisha umri wa miezi saba nane mpaka tisa ila dawa hizi uwa zinatofautiana kuna zingine za kujifusha au kunawa ukeni kwa ajili ya kuongeza nji na zingine kuoga ama kunywa ambapo nyingine tukizitumia kupaka kwenye tumbo kuelekea chini, dawa hizi zinatumika mara mbili kwa siku yaani Asubuhi na jioni
Lovenes Njinjo ni Mama aliejifungua Watoto Mapacha katika Kituo cha Afya Ruangwa ambae anakili kutumia Dawa hizo za Asili kabla ya kujifungua ambapo alieleza kuwa licha ya Watoto wake hao wawili kutanguliza miguu wakati wa kujifungua lakini alijifungua salama
“Mimi nilivyokuja hapa sijasumbuka sana kivile Nilitumia dawa tu za miti na majani nilinawa kabla ya kuja hivyo njia ilikuwa imejionyesha toka jana nilipokuja sema nilichukuwa muda kidogo kwa kuwa huyu mmoja ndio alikuwa anasumbua sana kumngojea mwenzie na hata alivyokuja huyo walianza kutanguliza miguu sio kichwa lakini wote walitoka salam”
Kwa upande wake Muuguzi Mkunga wa kituo cha Afya Ruangwa Tusajigwa Mwaisaka Alisema wakati Mwingine Watoto upoteza Maisha kutokana na kunywa maji hayo ya Dawa ambayo utumika na Mama zao kwa ajili ya kuongeza uchungu kabla ya kujifunguan
“tunaweza kumgundua Mama alietumia Dawa hizo za Asili kwa kumuangalia tumboni kuwa na rangi nyeupe nyeupe kwa Mama alie tumia Dawa za kupaka au pindi chupa ya maji ya uchungu inapovunjia na maji hayo kubadilika rangi kuwa ni ya kijani kwa Mama alietumia Dawa ya kunywa” alieleza Mwaisaka
Hata hivyo Mkunga huyo alitoa Rai kwa akina Mama kuacha mara moja matumizi ya dawa hizo kuwa hazina ukweli wowote kwa kuwa zinamadhara kwake na Watoto kwa ujumla kwani uchungu wa Mama wakati wa kujifungua unakuja kwa Asili sio kwa kutumia Dawa hizo
Ili kuhakikisha ukuwaji wa Mtoto haukumbani na changamoto yoyote tangu mimba inavyotungwa kuzaliwa na kukua kwake Serikali imekuja na mpango maalumu ujulikanao kama Program jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) Ikiwa na lengo la kuhakikisha maendeleo ya ukuwaji wa Watoto wote wa Tanzania yanapatikana ili waweze kufikia ukuwaji timilifu
Program hiyo itafanya kazi katika malengo mahususi ya muda mrefu ambayo yatashughulikia changamoto za kimfumo na kiprogramu zinazoathiri ukuwaji na maendeleo ya Watoto wadogo wenye umri kati ya 0-8 hapa Nchini
0 Comments