Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA SOKO LA MATUNDA DODOMA WATAKIWA KUPISHA UKARABATI

 


Na Hamida Ramadhana,Matukio Daima  APP Dodoma

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru ameendelea kuwataka wafanyanishara wa soko la matunda na Mbogamboga Sabasaba kupisha ukarabati wa soko hilo huku akieleza lengo la serikali ni jema kwa maslahi ya wafanyabaishara hao na siyo vinginevyo.


Hatua hiyo imekuja baada ya wafanyabiashara wa soko la Sabasaba jijini Dodoma kutishia kuandamana kwenda bungeni kumuona Waziri mkuu Kassim Majali ili kumfikishia kilio chao cha kuondolewa bila kushirikishwa mkurugenzi wa jiji hilo.


Akiongea na waandishi wa habari leo Aprili 20, 2022 amesema lengo la jiji ni kuwahamisha kwa muda ili kufanya ukarabati wa soko hilo na baada ya ujenzi huo kukamilika watawarudi kuendelea na shughuri zao kama kawaida.


Amesema lengo ni kufanya uhakiki na  kuwatambua nani anamiliki nini na anafanya nini  watarudi katika maeneo yao .


Aidha amesema soko hilo ni la historia na limechakaa na ni la muda mrefu tangia mwaka 1996 halijafanyiwa ukarabati miundominu yake ni mibovu .


"Dodoma Sasa ni Jiji na ndiyo Makao Makuu ya nchi na soko la Sabasaba limekuwa likilisha karibu Wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na ndio maana tunataka kufanya ukarabati .


Na kuongeza Kusema "Ndio Maana vua ikinyesha Mvua tope linakuwa la kutisha na nimekuwa nikipokea tunapokea simu za malalamiko kuwa tunachukua ushuru lakini hatufanyi ukarabati”amesema Mafuru


Amesema jiji halina lengo la kuwaonea wafanyabiasahara bali kinachotakiwa ni kuwashirikisha kila hatua ili kuweza kupata uelewa wa pamoja na kila mtu kuridhika na maamuzi hayo.


Hata hivyo amesema malalamiko ambayo wamekuwa wakiyapata yanaonyesha kuwa wafanyabiashara hao hawana imani na jiji katika kutekeleza mpango huo.


Amesema ili kupata kauli moja wanapanga kuendelea na vikao vya kujadilina baina ya jiji na uongozo wa soko hilo ili kupata namna bora ya kufikia mwafaka.


“Kuna watu wanahofu kupoteza vibanda vyao hasa wale wenye maeneo zaidi ya moja lakini ni wahakikishie kuwa kupitia mazungumzo tutafikia mwafaka na hakuna atakaye poteza haki yake waelewe tuu tunafanya uhakiki ili kujilidhisha na idadi ya wafanyabiasahara iliyopo”amesema


Kwa Upande wake Afisa Biashara ya Jiji la Dodoma Domitila Vedasto amesema soko la sababsa lina historia ya muda mrefu tangu mwaka 1996 waliahamishwa kutoka Nyerere Square na kupelekwa maeneo mbalimbali.


Pia amesema Soko la sababasa miundombini yake imechakaa na hata ukienda sasa hivi kuko wazi lakini pia hili ni jiji na makao makuu hatuwezi kuwa na soko la aina ile  kama jiji tukasema kuwe na kitu cha kufanya kuboresha soko kama hadhi ya jiji na kuendana na makao makuu ya nchi. 


"Tukawaza kuweka mkakati kwa maana katika mradi huu tutanza ujenzi mwezi wa saba na  huwezi kuanza bila kuwashirikisha wadau ,vikao vimeanza tangu mwaka jana kuhusiana na changamoto kikubwa miundombinu vikao vya kuanza kujenza tumeanza mwezi wa kwanza wtaalam walikuja tukawashirikisha," amesema Afisa Biashara .


Na kuongeza Kusema "Siyo kwamba hatuja washirikisha wafanyabiashara tumewashirikisha . hii ni picha kwamba tunawashirikisha jambo wana mambo yao wanaona kama vile tunawaona lakini kimsingi tunawasirikisha,'' amesema


Naye Mkuu wa idara ya Fedha Jiji la Dodoma Rahabu Philip, alisema siyo kweli kuwa wafanyabiashara hao hawajashirikishwa katika mpango huo wa jiji.


“Tumekuwa tukiwashirikisha wafanyabiashara toka mwaka jana na ujenzi huu unatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu baada ya serikali kutupatia fedha za kufanikisha ujenzi huu”amesema

Mwishoni mwa wiki iliyipita viongozi wa soko hilo wakizungumza na waandishi wa habari walidai kuwa wanapanga kufanya maandamano hadi Bungeni ili kufikisha kilio chao kwa waziri mkuu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI