Wafanyabiashara Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufuata kanuni na Sheria za vipimo kwani hatayebainika hakikiuka Sheria za vipimo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Ameyasema hayo meneja wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro Salim Masimbe wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi ambapo amesema kuwa tangu January mwaka huu wameshafanya vipimo vya wafanyabiashara zaidi ya elfu kumi na sita.
Meneja huyo amesema. zaidi ya wafanyabiasha elfu kumi wamefanyiwa uhakiki wa vipimo visivyo ikiwa ni moja ya hatua ya kudhibiti matumizi holela ya vipimo kwa wafanyabiashara.
Aidha amesema katika kaguzi hizo wamegundua kasoro mbalimbali za vipimo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutozingatiaji matumizi sahihi ya Mizani.
"Tumefanya kaguzi katika maduka ya vifaa vya ujenzi ( hadrwear )na tumegundua kasoro mbalimbali za kivipimo hasa kwenye sehemu hizo za maduka yanayouza vifaa vya ujenzi , tumegundua kwamba Kuna mapungufu katika kulebo vile vifaa kwa mfano labda paip haisemi ni mita ngapi inamuwiya mteja kujua ananunua kiasi gani"Alisema Masimbe.
Amesema kuwa mara bà ada ya kigundua mapungufu hayo walitoa elimu kabla kutoa adhabu ambapo pia Alisema walifika katika viwanda vinavyozalizalisha vifaa hivyo.
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wafanyabiashara ili kuhakikisha wanazingatia matumizi sahihi ya Vipimo na kusema Kuna faida za kutumia vipimo ikiwa ni pamoja na kupata faida katika bidhaa wanazoziuza na kununua.
0 Comments