Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.
Vyama vya ushirika kwa kushirikiana na Serikali kupitia wizara ya kilimo nchini imekusudia kuanzisha kuanzisha benki ya ushirika itakayosaidia kutoa mitaji kwa vyama vya ushirika baada ya vyama hivyo kukoswa mitaji kwaajiri ya kuendesha shughuli zao.
Hayo yamesemwa na kaimu mrajisi kutoka chuo cha ushirika Moshi Augustino Senkuruto katika mkutano mkuu uliofanywa na chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera Co-operative Union Limited (1990) uliofanyika katika ukumbi wa Yasila uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kusema kuwa, tume ya ushirika pamoja na wizara walikaa na kukubaliana kuanzisha benki hiyo ili kutatua changomoto mbalimbali zinazovikabili vyama vya ushirika zikiwemo ukosefu wa mitaji.
“Sisi kama tume ya maendeleo ya vyama vya ushirika tuliitana kwa kushirikiana na wizara ya kilimo kwaajiri ya kutafuta mtaji wa bil. 15 kwaajiri ya kuanzisha benki ya ushirika itakayosaidia kutoa mitaji kwenye vyama vya ushirika vipatavyo 9742 vilivyopo nchi nzima”
Aidha, amewataka wajumbe wa bodi katika vyama vya ushirika kufanya kazi kwa uhadilifu, maadili na weredi na kuweka tamaa zao pembeni.
“ Baadhi ya viongozi katika vyama vyetu wamekuwa sio waadilifu, ndugu wajumbe wote hapa ni viongozi tuko kwenye vyama vyetu vya ushirika bado suala la uhadilifu na maadili limekuwa ni tatizo linaendelea kutafuna vyama vyetu, sasa basi sisi kama tume ya Maendeleo ya ushirika tulishachukua hatua zaidi ya miaka mnne(4) mitano(5) na hapa kagera ni mfano mzuri, mimi nawaomba na nawasihi tufanye kazi kwa weredi, uhadilifu na maarifa tusiwe wabinafsi na tusiweke tama zetu mbele”
Kwaupande wake mwenyekiti wa chama kikuu cha uchirika KCU mkoani Kagera Ressy Mashulano amesema kuwa tangu walipochaguliwa kukiendesha chama hicho wameweza kutatua baadhi changamoto ambazo zilikuwa zikivikumba vyama vya ushirika pamoja na wakulima wa kahawa zikiwemo za kuchelewa kwa malipo.
“ Tumejitahidi kutekeleza kazi zetu kwa uhadilifu kadri tilivyojaliwa kwani tangu tulipochanguliwa mpaka sasa tumeweza kufanya mambo mbalimbali kama vile kulipa mkopo wa benki kwa wakati kwani katika msimu wa 2021/2022 KCU ilikopa pesa bil.9.5 kwaajiri ya kulipa malipo ya awali ya wakulima na kuhudumia gharama za zao hadi tarehe ya mkutano huu fedha hizo zote ikiwemo riba zimelipwa kwa wakati, sambamba na hilo tumeweza kufanikiwa kuwalipa mkulima wa kahawa kwa wakati na kwa muda usiozidi masaa 22 tangu kahawa inapofikishwa kiwandani au kwenye ghala letu kuu la kemondo na mpaka sasa hakuna mkulima anayekidai chama hiki fedha za kahawa”
Aidha amewaomba wajumbe wa mkutano mkuu kuidhinisha ya zaidi ya shilingi bil. 1 zilizopendekezwa ili zitumike kwaajiri ya ustawi wa jamii kwa vyama vya msingi,uendeshaji wa mazingira , ‘fair trade’, uzalishaji wa miche ya kahawa, uboreshaji wa miundo mbinu ya chama iliyochakaa, mwendelezo wa viwanja vya ushirika pamoja na utunzaji wa mashamba ya miti yanayomilikiwa na chama hicho kikuu cha ushrika.
0 Comments