Header Ads Widget

SERIKALI, WADAU WATAKIWA KUSAPOTI TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI

 



Na Fatam Ally Matukio Daima APP, Dar es Salaam


Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimaendeleo wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi zisizo za kiserikali ambazo zimelenga kuisaidia jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.



Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Nuru yetu Foundation Zauja Mohamed Roble wakati alipokua katika Mkutano wa Girls Round Table msimu wa nne ambapo amesema kuwa lengo lao ni kufikia vijana wengi katika mikoa mbalimbali.


"Tunaiomba Serikali pamoja na wadau mbalimbali wajitokeze kutuunga mkono juhudi tunazifanya ambazo zimekua zikitoa matokeo chanya katika jamii, kwani lengo letu ni kuisaidia jamii kuzifikia ndoto zao"amesema Zauja.



Amesema kuwa, kwa sasa Girls Round Table inafanyika jijini Dar es Salaam kwa misimu minne mfululizo, lakini lengo lao kuweza kufukia vijana wengi zaidi katika mikoa yao, hivyo ni vyema Serikali kuwekeza katika taasisi hizo.


"Kwani wanapokutana pamoja wasichana kuna vitu vingi ambayo wanaweza kujifunza, tunawakutanisha na watu waliofanikiwa kimaisha kwa kukabiliana na changamoto ambazo, hawawezi kutoka watupu, wanajifunza mengi sana"amesema Zauja.


Akielezea safari yake ya mafanikio, Msaniii wa Hiphop nchini Tanzania Kala Jeremiah amesema Ili uweze kufanikiwa katika safari yako ni lazima uwe na msimamo na usibadilishe mawazo kwa vitu unavokutana njiani, huku akiwataka mabinti kujiamini katika vitu ambayo wanavifanya Ili kuweza kutimiza ndoto zao.



"Katika maisha kuna changamoto nyingi lakini kwa upande wenu wanawake zimezidi maana anaweza akatokea mwanaume ukampenda na ukabadilisha kila kitu katika maisha yako, akikuacha tu unaharibikiwa, lazima uwe na msimamo wako , utafanikiwa"amesema Kala.


Aliongeza kuwa"nilichelewa kutoka kimaisha kutokana na misimamo yangu, sikutaka mtu anichagulie njia ya kupita, nilipitwa na mambo mengi lakini sikukata tamaa nilipambana kufanya jambo ambalo niliona linafaa, kwa sababu niliingia kwenye mziki kuisaidia jamii na sio kuwa maarufu"amesema.



Nae, mchekeshaji Mc Mboneke amesema lengo la kuwepo katika Girls Round Table ni kutoa hamasa kwa wasichana waweze kutimiza ndoto zao, na kujifunza kutoka watu ambao wamefanikiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI