Header Ads Widget

NAPE AUPA TANO MKOA WA LINDI KWA KUFANYA VIZURI ZOEZI LA ANUANI ZA MAKAZI NA POST CODE

NA HADIJA OMARY ,MATUKIO DAIMA APP LINDI 

WAZIRI wa Habari, Teknolojia na mawasiliano Nape Nnauye  ameupongeza mkoa wa Lindi kwa kufanya vizuri katika zoezi la uwekaji wa Anwani za makazi na Post Code na kubaki katika nafasi kumi bora kwa mikoa yote nchini Tanzania tangu kuanza kwa zoezi hilo.

Ameyasema hayo akiwa katika  ziara ya ukaguzi wa zoezi hilo mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa zihara yake ya kukagua zoezi la uwekaji anuani za Makazi Nchi Mzima 

Waziri Nape alitumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi na wananchi  wa Mkoa huo kwa  ushirikiano waliouonyesha kwani  kufanya vizuri kwa Mkoa huo ni heshima kwake kwa kuwa jimbo lake lipo Mkoa wa Lindi.


"nafasi ya Mkoa kufanya vizuri, katika zoezi hili la anuani za makaazi  limeniheshimisha  kwanza mimi mwenyewe kama Mbunge wa jimbo la Mtama linalopatikana katika Mkoa  huu wa Lindi Pamoja na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ambaye ni Mwenyekiti wa kamati inayoendesha na kuratibu zoezi la Anwani na Post Code hapa  Nchini.

Aidha Waziri Nape amewataka viongozi kufanya maamuzi ya kutoa Majina ya mitaa yatakayoenzi Historia ya Mkoa na viongozi mbalimbali licha ya wananchi kuwa na nafasi ya kupendekeza majina ya mitaa yao.

Awali Mkuu wa wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack, akieleza mwenendo wa zoezi la uwekaji wa anuani za Makaazi na post code  alisema kuwa zoezi wakati zoezi hilo linaendelea  mbali na kutengeneza ajira kwa vijana waliohusika , pia imesaidia kujenga mahusiano na taasisi zingine.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI