.
Na, Titus Mwombeki-MATUKIO DAIMA APP BUKOBA.
Wazazi wenye watoto chini miaka 5 mkoani kagera na Tanzania kwa ujumla wametakiwa kukaa tayari ili watoto wao wapatiwe chanjo ya polio itakayotolewa kwanjia ya matone nyumba kwa nyumba, ili kusaidia kurahiusisha zoezi la utoaji wa chanjo hiyo itakayosaidia kuimalisha kinga ya watoto hao dhidi ya ungonjwa huo baada ya mgonjwa mmoja wa ugonjwa huo kugundulika nchi Malawi.
Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wahuduma za chanjo Kagera Zablon Segeru katika kikao maalumu kilichoandaliwa mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali Charles Mbuge kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa kagera pamoja na viongozi mbali mbali wa ulinzi na usalama na dini kwa lengo la kuhamasishana na kuweka mipango madhubuti jinsi ya kufanikisha kampeni ya chanjo ya polio inayotegemewa kuanza tarehe 24 na 25 mwezi huu kitaifa.
“ Ugonjwa wa polio ni ugonjwa unaosababisha na kupooza au ulemavu wakudumu na kimsingi unaweza kulekea hadi kifo, chanjo pekee ndiyo tiba ambayo inaweza kumsaidia na kumlinda mtoto au watoto ili wasiweze kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu”
Aidha, amesema kuwa jamii inatakiwa kuelewa umuhimu na faida mbalimbali zinatokana na chanjo hii yenye lengo la kuimarisha kinga ya mtoto, itakayo itatolewa kwa awamu ili kunusuru maisha ya watoto wao kwani chanjo hii ni salama na haina madhara yoyote.
Kwaupande wake afisa elimu mkoa wa Kagera Khalifa Shemahonge akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Generali Charles Mbuge amesema kuwa viongozi wote wa hasa wamitaa wanatakiwa kuelimishwa juu ya umuhimu wa chanjo hii ili nao waweze kuelimisha wananchi wanaowaongoza kufanikisha zoezi.
“Kila mtu hapa amejua wajibu alionao juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huu hatari, hivyo basi niwaombe viongozi wanaoongoza makundi mbalimbali hasa viongozi wa dini wana habari pamoja na viongozi wa mitaa wapatiwe elimu juu ya umuhimu wa chanjo hii nao pia wakaelimishe jamii zao umuhimu huo ili kufanikisha kampeini hii ambayo ni kitaifa”
Takwimu zinaonyesha kuwa nchi ya Tanzania iliripoti kisa cha mgonjwa wa polio kwa mara ya mwisho mwaka 1996, lakini zimekuwepo nchi ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na Afghanistan, Pakstani pamoja na Malawi ambao wametangaza kisa kipya hivi karibuni.
0 Comments