Header Ads Widget

NAPE AHIMIZA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI LITUMIKE KUWAENZI WABUNIFU NA WAASISI MBALIMBALI NCHINI.

 



Teddy Kilanga _Arusha


Waziri wa habari,maasiliano na Teknolojia ya habari,Nape Nnauye amewataka wananchi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali mkoani Arusha kutumia zoezi la anwani za makazi kuwaenzi waasisi na wabunifu ili kulinda historia yao.



Waziri Nape alisema hayo katika ziara yake ya kukagua zoezi la anwani za makazi mkoani Arusha ambapo ameelekeza kuangalia njia ya kutumia zoezi hilo kuenzi historia ya nchi kwa kutaja majina viongozi na wabunifu katika maeneo yao ya mitaa na barabara kubwa kutokana na utendaji kazi wao katika kutengeneza historia ya nchi.



"Kumekuwa na changamoto za baadhi ya maeneo ya majiji kuwa kelele za majina yanayotumika katika mitaa yetu hivyo napenda kutoa wito kuangalia uwezekano wa kuenzi historia ya nchi hii kwenye kutaja majina ya barabara zetu na mitaa,"alisema.



Waziri alisema pamoja na watu wengi na misaada wanayosaidia isiwe msingi  wa kutaja majina ya mitaa na barabara hivyo awaomba viongozi wa mkoa wa Arusha na wananchi kutumia fursa hiyo kuweka historia vizuri kwani wapo Mawaziri wakuu wengi katika nchi ni vyema wakaenziwa.



Vilevile alisema wapo watu waliofanya ubunifu mkubwa ili kulinda historia yao isipotee katika nchi hivyo anaomba mkoa wa Arusha kuwa mfano katika hilo pamoja na kutumia mfumo katika kujiridhisha na data zinazotolewa katika mitaa.



Aidha Mongella alisema zoezi la makazi ni fursa kwa watalii wanaofika kutalii nchini ambapo itawasaidia kuwaelekeza maeneo husika wanayoyatembelea ambapo ndani ya mfumo huo kutakuwa na lugha mbalimbali za kimataifa.



Nape alisema changamoto za kimfumo  wataendelea kuongeza nguvu huku wakiendelea kukamilisha zoezi la anwani za makazi nchini ili wasimuangushe Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kutimiza lengo la serikali.



Aidha Waziri Nape amewaagiza Wakala wa barabara mijini(Tanroad) na wakala wa barabara vijijini (Tarura) kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili liweze kukamilika kwa wakati.



Hata hivyo Waziri Nape ameupongeza uongozi wa mkoa wa Arusha kwa kuwa na karakana ya vifaa vya utumiaji katika zoezi la Makazi kwani wameisaidia serikali katika kupunguza gharama za uendeshaji wa zoezi hilo hivyo anawataka mikoa mingine kuiga mfano huo.




Kwa upande wake Katibu tawala Msaidizi wa mkoa wa Arusha,Said Mabiye amesema mkoa wa Arusha umeshapokea takribani sh.milioni 905.1 kwa ajili ya halmashauri zote kuweza kutekeleza zoezi hilo.



"Katika zoezi hilo jiji la Arusha limefikia katika hatua asilimia 78.72,halmashauri ya Monduli asilimia 45.82,Longido asilimia 39.04,Ngorongoro asilimia 12.51 ,Arusha asilimia 11.21,Meru asimia 4.21 na Karatu  ni asilimia 2.



Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella alisema zoezi hilo mkoani hapo linatarajiwa kukamilika mnamo Aprili 30,2022 hivyo wataongeza juhudi na umakini katika kukamilisha kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI