Header Ads Widget

KAPOLE, MSIWAFICHE WATU WENYE ULEMAVU NDANI WAKATI WA ZOEZI LA SENSA NA MAKAZI.

 



NA CHAUSIKU SAID _MWANZA


Jamii imeshauriwa kutowaficha watu wenye ulemavu wakati wa zoezi la sensa ya watu na makzi kwani na wao wana haki ya kuhesabiwa kama watu wengine wasio na ulemavu.



Mwenyekiti wa chama cha shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Alfred Kapole ameeleza kuwa watu wasiwafiche watu wenye ulemavu wa aina yeyote ile na wasiachwe nyuma katika zoezi hili kwani kila mmoja anapaswa kufahamu haki zake za msimgi.



Kapole ameeleza kuwa jamii inapaswa kuendelea kuhamasishwa na kupewa elimu  ya kutosha juu ya umuhimu wa sensa pamoja na watu wenye ulemavu wenyewe kuwa mstari wa mbele na kutoa ushirikiano wa kuyosha na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.



"Kama watu wenye ulemavu wakiwaficha ndani hata serikali haitaweza kufahamu mahitaji yao ya msingi na hata wakifahamu ni kwa watu wachache walioweza kutambuliwa hivyo basi tusiwanyime haki ya msingi watu hawa" Alisema Kapole.



Kutokana na serikali kuona kuna haja ya kuwasidia wenye ulemavu katika zoezi hilo pia wenye ulemavu na wao wanapaswa kuongeza juhudi za kusambaza taarifa ili kipindi cha zoezi hili linapokaribia kufanyika kusiwe na wasiwasi ya watu wengine kutohesabika.



Kapole amesema kuwa kuna haja ya serikali kutoa elimu ya lugha ya alama  kwa watu watakaofanya zoezi la hilo la sensa na makazi ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa ufasaha na watu wenye ulemavu kupata haki yao.



"Ni lazima kuwe na lugha ambayo ni faraja kwao unakuta mtu ni mwenye ualbino ila kwa sababu mtu hafahamu ni namna gani mtu wa namna hiyo anapaswa kiutwa ndio ile unasikia huyu ni mlemavu wa ngozi" alisema Kapole.




Hata hivyo ameeleza kuwa kila mmoja ana umuhimu wa kushiriki kwenye zoezi hilo la sensa na kufanya hivyo kutaisaidia serikali kupanga bajeti kutokana na kifahamu wananchi wao wako wangapi kuliko kukadilia.



" kimsingi hata ukiangalia vitabu vitakatifu vinasema kipindi cha yesu kuzaliwa watu walihesabiwa hivyo basi kuhesabiwa ni haki ya kimsingi" Alisema Kapole.



Aidha aliongeza kuwa jamii bado inanafsi kubwa ya kutoa elimu kwa wale ambao hawajafahamu nini maana ya sensa ya watu na makazi ili waweze kufahamu jambo hilo na sio kuiachia serikali peke yake iwajibike kutoa elimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI